Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 January 2015
Tuesday, January 06, 2015

Tetesi za Usajili zinaendelea kwa Liverpool


 Na Oscar Oscar Jr

Kuna habari zilizopatikana leo kutoka magazeti ya Uingereza yakimtaja kocha Rafael Benitez kurejea kwenye klabu yake ya zamani ya Liverpool na hii ni kutokana na kocha wa sasa Brendan Rodgers kuonekana kutokuwa na mwenendo mzuri tangu kuanza kwa msimu huu ambapo michezo 20 imeshapigwa mpaka sasa.

Kwa upande wa usajili, Rodgers anapigana usiku na mchana kupata mshambuliaji ambaye atakuja kufufua matumaini kwa klabu hiyo kuweza kurejea kwenye michuano ya Ulaya ambayo msimu huu wametolewa mapema kabisa huku Saido Berahino na Wilferd Bonny wakitajwa kuelekea kwenye klabu hiyo.

Berahinho ndiyo mchezaji ambaye anaweza kujiunga na Liverpool na hii inathibitisha na namna mchezaji huyo alivyoanza kuonyesha hali ya kutofurahia tena maisha akiwa na West Bromwich Albion.

Kitendo chake cha kutoshangilia hata bao moja kwenye ushindi wa mabao 7-0 ambapo alifunga mabao manne kwenye mchezo huo wa kombe la FA mzunguko wa tatu, ni ishara tosha kuwa anataka kutimka ingawa Liverpool watapata upinzani kutoka kwa klabu ya Tottenham Hotspurs.

Kwa upande wa Bonny kunaonekana kuwa vigumu kwa Liverpool baada ya mshambuliaji huyo raia wa Ivory Coast kudai hivi karibuni kuwa angependa kujiunga na timu ambayo inauhakika wa kushiriki michuano ya klabu bingwa Ulaya.

Manchester City ambao ndiyo mabingwa watetezi wa ligi kuu Uingereza, wameonekana kumfungia kazi mchezaji huyo hasa baada ya washambuliaji wake Eden Dzeko na Kun Aguero kuwa majeruhi. 

Kama Manchester City wakikaza kamba, mchezaji huyo atajiunga nao muda si mrefu. Liverpool ambao wako kwenye nafasi ya nane kwenye ligi kuu, bado hakuna uhakika kama watamaliza ndani ya nne bora.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!