John Terry atema maneno ya kutia moyo.
Na Oscar Oscar Jr
Nahodha wa timu ya Chelsea, John Terry ameibuka na kuzungumza maneno ya busara ambayo yanatosha kuwa faraja kwa mashabiki na wapenzi wa klabu ya Chelsea baada ya kupata kichapo cha mabao 5-3 mbele ya timu ya Tottenham Hotspurs siku ya mwaka mpya.
Nahodha huyo amesema kuwa, kipigo hicho hakikumfurahisha kila mtu na baada ya mchezo huo walikutana kwenye vyumba vya kubadilishia nguo na kuzungumza namna ya kusahau kichapo hicho wao kama wachezaji na kushikamana kuelekea michezo mingine inayofuta na kuhakikisha wanarejesha vipindi vya furaha kwenye kikosi hicho cha kocha Jose Mourinho.
Chelsea bado wanakamata nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa ligi kuu licha ya kufungamana na mabingwa watetezi wa ligi hiyo, Manchester City ambao mara baada ya kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Sunderland waliweza kuwafikia Chelsea kwa kufikisha pointi 46.
John Terry akizungumza kupitia mtandao wa klabu hiyo, ameleleza wasiwasi wa kufungamana na Manchester City ambao hapo awali walikuwa wamewazidi pointi nane na sasa wamelingana kwenye kila kitu huku Diego Costa naye akimfikia Sergio Aguero kwa kufunga mabao 14 ya ligi hiyo ambayo inaelekea kuwa na ugumu kwenye mechi 18 zilizosalia.
Timu hizo kwa sasa zote zina pointi 46, zimeruhusu kufungwa mabao 19 huku kila moja ikiwa na magoli 44 ya kufunga. Kinachofanya Chelsea kubaki kileleni ni herui ya kwanza kwenye timu hiyo.
Manchester United wanaendelea kubakia kwenye nafasi ya tatu baada ya kulazimisha sare ya bao 1-1 dhidi ya Stoke City huku Southampton wakiendelea kupigania nafasi ya nne kwa kuwachapa Arsenal bao 2-0.
0 comments:
Post a Comment