Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 January 2015
Tuesday, January 06, 2015

Habari njema kwa Manchester United.


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye klabu ya Manchester United imewasilisha ombi rasmi la kumuhitaji beki wa kati wa kimataifa wa Ujerumani na klabu ya Borussia Dortmund, Mats Hummels kwa mujibu wa mtandao wa Tutto Mercato.

Hii inaweza kuwa habari njema kwa mashabiki wa Manchester United ambao wamekuwa na upungufu kwenye eneo hilo hasa baada ya kuondokewa na walinzi wake Rio Ferdinand na Nemanja Vidic mwishoni mwa msimu uliopita.

Kwa upande wa pili, Manchester United wamekuwa wakihusishwa na kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Uholanzi tangu enzi wa Sir Alex Ferguson bila mafanikio na dirisha hili, bado wameendelea kumfukuzia kiungo wa Galatasaray, Wesley Sneijder japo Juventus ndiyo wenye uwezekano wa kumnasa.

Maisha ya mshambuliaji Javier Hernandez ndani ya Old Trafford yanaonekana kufikia ukingoni baada ya taarifa zilizotoka leo kuelezea kuwa hakuna namna mshambuliaji huyo raia wa Mexico ataweza kurejea tena Old Trafford.

Taarifa zimeeleza kuwa endapo United watamkosa Radamel Falcao kwa uhamisho wa kudumu, kocha Loius Van Gaal atahitaji mshambuliaji mwingine na sio Chicharito.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!