Na Chikoti Cico
Prince Ali Bin Al Hussein kutoka familia ya kifalme nchini Jordan na ambaye pia kwasasa ni makamu wa Raisi wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) huku pia akiliongoza shirikisho la soka la Jordan na Mashariki mwa bara la Asia, ametangaza nia ya kugombania nafasi ya uraisi wa FIFA katika uchaguzi utakaofanyika mwezi Mei mwaka huu nchini Uswisi.
Prince huyo ataungana na Jermone Champagne kwenye kinyang’anyiro hicho cha uraisi wa FIFA dhidi ya raisi wa sasa Sepp Blatter ambaye anatarajia kutangaza nia ya kugombania uongozi huo kwa mara ya tano toka alipochaguliwa mwaka 1998.
Akielezea nia yake ya kugombania uraisi wa FIFA Prince Ali alisema “nautafuta uraisi wa FIFA kwasababu naamini ni muda wa kubadilisha mtazamo kutoka kwenye mgagaziko wa utawala na kurudi kwenye mchezo.
Huu haukuwa uamuzi rahisi umekuja baada ya kufikiria kwa makini na majadiliano mengi na washirika wa heshima wa FIFA kwa miezi michache iliyopita”
“Ujumbe niliousikia mara kwa mara ni kwamba ni muda wa mabadiliko, mchezo wa dunia unastahili uongozi bora, shirikisho la kimataifa ni shirika la huduma na mfumo wa maadili, uwazi na utawala bora”
Uongozi wa FIFA chini ya Blatter umekumbwa na kashfa nyingi za rushwa hasa kwenye kinyang’anyiro cha kutafuta waandaji wa kombe la Dunia kwa mwaka 2018 na 2022 ambapo Urusi na Qatar zilishinda.
0 comments:
Post a Comment