Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 January 2015
Friday, January 02, 2015

Simba yaanza vibaya Mapinduzi Cup.


Na Oscar Oscar Jr

Bao pekee lililofungwa na kiungo wa zamani wa Simba Sc, Henry Joseph lilitosha kuwapatia ushindi vijana wa Mtibwa Sugar kwenye kombe la Mapinduzi linaloendelea huko visiwani Zanzibar mbele ya wekundu wa Msimbazi timu ya Simba.

Mtibwa ambao ndiyo vinara wa ligi kuu Tanzania bara, waliweza kujipatia bao hilo pekee ambalo limeonyesha mwanga mzuri kwao. Simba ambao walifunga mwaka vibaya kwa kuchapwa na Kagera Sugar kwa bao 1-0, wamefungua mwaka vibaya pia kwa kichapo cha aina hiyo kutoka kwa vijana wa kocha Mecky Mexime.

Simba ambayo ilikuwa chini ya kocha msaidizi Suleimani Matola ambaye alikiongoza kikosi hicho baada ya kocha mkuu, Patrick Phiri kuwa safarini kuelekea Zambia kwa kile kinachodaiwa kuwa maisha ya kocha huyo na wekundu wa Msimbazi yanaweza kuwa yamefikia mwisho.

Simba ambayo inaonekana kusua sua, imegeuka kuwa mteja kwa Mtibwa Sugar baada ya timu hizo kukutana mara tatu hivi karibuni huku Simba ikijikuta ikichezea vichapo mara mbili na kutoka sare mara moja. 

Matatizo ya Uongozi ni moja ya sababu kubwa zinazochangia timu hiyo kushindwa kutamba kwa miaka miwili ya hivi karibuni. Uongozi mpya wa Rais Evance Aveva, umeonekana kuleta makundi makubwa ndani ya timu huku kukiwa na habari za kuwapendelea wachezaji wa kigeni ambao msimu huu wote wanatoka Uganda.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!