Searching...
Image and video hosting by TinyPic
1 January 2015
Thursday, January 01, 2015

Lampard aibeba Manchester City.


 Na Oscar Oscar Jr

Mfungaji bora wa muda wote wa Chelsea ambaye kwa sasa anakipiga na klabu ya Manchester City Frank Lampard kwa mara nyingine jana aliweza kuwa shujaa wa mchezo pale alipofunga bao la ushindi dakika ya 73 mbele ya Sunderland ambao walionekana kupambana angalau waondoke na lama moja.

Mchezo huo uliopigwa kwenye dimba la Etihad, ulishuhudia magoli matano yakizama wavuni huku kwa upande wa Manchester City Yaya Toure, Steven Jovetic na Lampard wakifunga na kwa upande wa Sunderland, Jack Rodwell 68′ na Johnson 71′ (pen)waliweza kuingia kwenye orodha ya wafungaji.

Manchester City ambao walionekana kuutawala mchezo, walifanikiwa kupiga langoni mwa Sunderland mashuti 12 idadi ambayo hakuna timu ya ligi kuu imefanya msimu huu huku Lampard akionekana kuwa kwenye uwezekano hata wa kufunga magoli matatu.

Matokeo hayo yanawafanya mabingwa hao watetezi kula sahani moja na Chelsea ambao walichapwa na Spurs kwa bao 5-3 na kuwafanya wapoteze mchezo wao wa pili msimu huu baada ya hapo awali kufungwa na timu ya Newcastle United.

Goli hilo la Lampard linamfanya kiungo huyo wa kimataifa wa zamani wa Uingereza kutimiza magoli tisa ambayo ameshaifunga timu ya Sunderland. 

Lampard ambaye mkataba wake wa mkopo akitokea klabu ya New York City ulimalizika Desemba 31, 2014, ameongeza mkataba na sasa atakuwa na Manchester City hadi mwisho wa msimu huu.

Kwa upande mwingine, Manchester United walitoka sare ya 1-1 na Stoke City huku Stoke wakifunga kupitia kwa Ryan Shawcross na Falcao akasawazisha kwa upande wa United. 

Arsenal walichezea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Southampton huku magoli hayo yakifungwa na Saido Mane na Dusan Tudic.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!