Na Chikoti Cico
Taarifa kutoka nchini Uingereza zinasema kiungo na nahodha wa timu ya Liverpool, Steven Gerrard anatarajia kuiacha timu hiyo mwishoni wa msimu huu baada ya kuichezea kwa miaka 26 huku akiiongoza kama nahodha kwa zaidi ya miaka 11.
Gerrard ambaye mkataba wake unaisha mwishoni mwa msimu huu na ambaye amekuwa na mazungumzo ya muda mrefu na Liverpool kuzungumzia kupewa mkataba mpya, kwasasa yuko huru kuanzisha majadiliano na klabu nyingine na pia anaweza kusaini mkataba na klabu nyingine utakaoanza kufanya kazi mwishoni mwa msimu.
Akiwa ameichezea Liverpool michezo 695 kuna taarifa zinasema tayari kiungo huyo ameanza mazungumzo na klabu za Los Angeles Galaxy, New York City na Red Bulls za nchini Marekani ili aweze kusajiliwa na moja ya klabu hizo kwenye kipindi cha majira ya joto, pia timu kutoka Asia na sehemu zingine za Ulaya zimeonyesha nia ya kumsajili Gerrard.
Baada ya taarifa za kuondoka kwa Gerrard mwishoni mwa msimu kutoka nahodha na beki wa zamani wa Liverpool Jimmy Carragher ambaye aliwahi kucheza pamoja na Gerrard aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kwamba
“ni siku ya huzuni kwa Liverpool na soka la Uingereza kwa taarifa za Gerrard lakini nafikiri ni uamuzi sahihi mambo yote yakizingatiwa”
Huku akiwa ameifungia Liverpool magoli 177 na kushinda vikombe 10 vikubwa na klabu hiyo, Gerrard anaondoka huku akiwa hajafanikiwa kunyakua kombe la ligi kuu nchini Uingereza maarufu kama “Barclays Premier League” katika miaka yake 26 aliyoichezea klabu ya Liverpool.
0 comments:
Post a Comment