Sheria yambeba Bosi wa Bayern Munich
Na Oscar Oscar Jr
Aliyekuwa Chifu wa klabu ya Bayern Munich ya nchini Ujerumani, Uli Hoeness amepunguziwa adhabu na sasa amepewa ruhusa ya kuwa uraiani muda wa mchana na inapofika jioni anatakiwa kuwa Gerezani ambapo anatumikia kifungo cha miaka mitatu na nusu.
Bosi huyo wa Mabingwa wa Ujerumani, alitiwa hatiani mwezi machi mwaka jana baada ya kushitakiwa kwa makosa ya kukwepa kodi kutoka mamlaka ya mapato ya nchini Ujerumani ambapo alidaiwa kukwepa mamilioni ya Euro na kulitia taifa hasara.
Kufuatia sheria hii ambayo inatumiwa na Wajerumani, Uli Hoeness anaruhusiwa kuajiriwa lakini ni lazima arudi Gerezani kabla ya saa 12:00 Jioni. Uli alitiwa hatiani baada ya kugundulika kuwa amekwepa kodi ambayo ingeweza kuliingizia taifa la Ujerumani Euro 28.5M.
Wakati hayo yote yakitokea, Bayern Munich imekuwa timu isiyokamatika chini ya kocha Muhispania, Pep Gaurdiola kwenye ligi ya Bundesliga ambapo wameendelea kuongoza pasipo kupoteza mchezo wowote huku wakiwa tayari wamejikusanyia pionti 45 katika michezo 17.
0 comments:
Post a Comment