Steven Gerrard apewa nafasi timu ya EPL.
Na Oscar Oscar Jr
Kiungo na mkongwe wa Liverpool, Steven Gerrard hatimaye maisha yake ya soka na klabu ya Liverpool yamefikia ukingoni baada ya klabu hiyo kushindwa kufikia makubaliano ya mkataba mpya ambapo mkataba wa sasa wa mchezaji huyo unatarajia kumalizika mwishoni mwa msimu huu.
Baada ya kiungo huyo kutangaza kuwa asingependa kwenda kwenye klabu yenye matarajio makubwa, kocha wa Southampton Mdachi, Ronald Koeman ameibuka na kusema kuwa endapo Gerrard atabadilisha mawazo na kuamua kubaki kwenye ligi kuu ya Uingereza nafasi ipo Southampton kwa ajili yake.
Kocha huyo ambaye ameiongoza Southampton hadi kwenye nafasi ya nne msimu huu baada ya mechi 20, amesema hata siku moja hawezi kusita kumpokea mtu wa aina ya Steven Gerard.
Kwanza ni kutokana na umuhimu wake katika safu ya kiungo na pili, ni kiongozi baada ya kuwa nahodha wa timu ya Taifa ya Uingereza na Liverpool kwa muda mrefu.
0 comments:
Post a Comment