Huu ndiyo mtihani mgumu kwa Carlo Ancelotti.
Na Oscar Oscar Jr
Mabingwa wa Kombe la Dunia kwa ngazi ya vilabu, Real Madrid wanakabiliwa na mwezi mgumu sana wa January baada ya kuwa na mechi tisa ngumu ambapo zipo zitakazo amua muelekeo wa timu kwenye mbio za mataji msimu huu.
Real Madrid wataanza kampeni yao ya mwaka mpya kwa kucheza na Valencia ugenini mchezo wa La Liga na kufuatiwa na mchezo wa Kombe la Mfalme ugenini pia dhidi ya Atletico Madrid kisha, Espanyol kwenye La Liga.
Real Madrid ambao wameshuka dimbani mara 22 mfululizo bila kupoteza mchezo wowote wa Ushindani ukiachilia mbali kichapo cha bao 4-2 walichopata kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Ac Millan, watakuwa na ugumu na kuwatoa watu wasiwasi kama watamaliza mwezi wa January wakiwa bado hawajang'oka kwenye mataji wanayogombea msimu huu.
Kwa mujibu wa ratiba ya kombe la Mfalme, endapo Real Madrid watawatoa Atletico Madrid hatua inayofuata watakuna na Barcelona kuelekea kutinga nusu fainali ya michuano hiyo na huu ni mtihani mwingine January hii.
Lengo kuu msimu huu kwa Real Madrid ni kujaribu kutetea ubingwa wa klabu bingwa Ulaya ambao umeonekana kuwa mfupa mgumu kwa vilabu mbalimbali ambavyo vimewahi kuwa kwenye ubora wa hali ya juu kama Barcelona ya Pep Gaurdiola na Bayern Munich ya Juup Heyncheys.
Pamoja na kucheza mechi 15 huku timu nyingine isipokuwa Sevilla zikicheza mechi 16, bado Real Madrid ipo kileleni mwa msimamo wa ligi kuu Hispania wakiwa na alama 39, wakifuatiwa na Barcelona wenye alama 38 na Atletico wakiwa nafasi ya tatu baada ya kupata alama 35 na leo watakuwa dimbani kucheza na timu ya Levante.
0 comments:
Post a Comment