Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 January 2015
Friday, January 02, 2015

Rekodi ya Real Madrid iko pale pale.


Na Chikoti Cico

Timu ya Real Madrid kutoka nchini Hispania wanaifukuzia rekodi ya kushinda michezo 24 mfululizo inayotambuliwa na kitabu cha rekodi duniani cha Guinness, mpaka sasa rekodi hiyo inashikiliwa na klabu ya Coritiba inayoshiriki ligi ya nchini Brazili.

Madrid ambao walifungwa kwa magoli 4-2 na AC Milan kwenye mchezo wa kirafiki uliofanyika Dubai Jumanne ya wiki iliyopita wanaendelea kuikaribia rekodi hiyo pamoja na kufungwa huko kwasababu mchezo huo wa kirafiki haukuwa mchezo wa kimashindano hivyo hautambuliki na kitabu cha Guinness.

Mpaka sasa Madrid wameshinda michezo 22 mfululizo ya mashindano mbalimbali huku mwishoni mwa mwezi Desemba wakifanikiwa kunyakua kombe la Dunia ngazi ya klabu kwa kuifunga klabu ya San Lorenzo kwa magoli 2-0 kwenye mchezo wa fainali nchini Morocco.

Coritiba inayoshiriki ligi ya nchini Brazili ndiyo inayoshikilia rekodi ya kushinda michezo 24 mfululizo kati ya mwezi Februari na Mei katika mwaka 2011.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!