Searching...
Image and video hosting by TinyPic
2 January 2015
Friday, January 02, 2015

Mourinho hakosi cha kusema kila anaposhindwa!




Na Chikoti Cico

Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho kwa mara nyingine tena amlalamikia mwamuzi baada ya timu yake kupokea kipigo cha magoli 5-3 dhidi ya Tottenham Hotspur kwenye mchezo wa ligi kuu nchini Uingereza uliofanyika kwenye uwanja wa White Hart Lane.

Baada ya kutoka sare ya 1-1 na Southampton kwenye mchezo uliopita Mourinho alimlalamikia Anthony Taylor ambaye alikuwa mwamuzi wa mchezo huo kwa kuinyima Chelsea penati ya wazi baada ya Fabregas kuangushwa kwenye eneo la hatari huku akienda mbali na kusema kwamba kuna “kampeni” ya kuinyima penati Chelsea kutoka kwa waamuzi.

Na baada ya Chelsea kupokea kipigo toka Spurs siku ya jana Mourinho kwa mara nyingine tena alimgeukia mwamuzi wa mchezo huo Phil Dowd kwamba alichangia matokeo kwenda hovyo kwa upande wa timu hiyo.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya mchezo huo Mourinho alisema “ninashtushwa na mambo mengine kuliko kufungwa magoli matano, ninashtushwa kwamba ndani ya siku tatu tumekuwa na maamuzi mawili ya kushangaza ambao yalituadhibu katika namna mbaya sana”

“Eden Hazard aliniambiwa kulikuwa hakuna adhabu wala kadi nyekundu alipochezewa vibaya kwenye kipindi cha pili lakini Mr Dowd alikuwa taratibu sana kwenda na mpira, alikuwa umbali wa yadi 40, alifanya uamuzi sahihi hivyo hilo ni zuri lakini alishindwa kufanya uamuzi ambao ulikuwa mita 10 tokea alipo kwenye kipindi cha kwanza, wakati muhimu wa mchezo”

Mourinho akiendelea kuonyesha kugadhabika kwa maamuzi ya mwamuzi huo aliendele kusema “matokeo yakiwa 1-0 tendo moja lililo wazi lingeweza kufanya iwe 2-0, matokeo na historia ya mchezo ingekuwa tofauti, meneja na wachezaji tunashinda na kupoteza lakini Mr Dowd hakupoteza, huu ni uamuzi ambao ni ngumu kuukubali”

Matokeo hayo dhidi ya Spurs yameifanya timu ya Chelsea kushika uongzo wa ligi pamoja na Manchester City ambao walishinda mchezo wao dhidi ya Sunderland kwa magoli 3-2 na kufikisha alama 46 sawa na Chelsea.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!