Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 January 2015
Wednesday, January 28, 2015

Ni Chelsea dhidi ya Spurs Wembley.


Na Chikoti Cico

Baada ya klabu ya Chelsea kuichapa timu ya Liverpool kwa jumla ya magoli 2-1 katika michezo miwili ya nusu fainali ya kombe la Capital One na kuingia fainali hatimaye klabu ya Tottenham Hotspur nayo pia imeingia fainali baada ya kuitupa nje ya kombe hilo klabu ya Sheffield United.
Spurs wameingia fainali baada ya kuifunga Sheffield United kwa jumla ya magoli 3-2 baada ya kushinda mchezo wa kwanza wa nusu fainali kwenye uwanja wa White Hart Lane kwa goli 1-0 wiki mbili zilizopita kabla ya kutoka sare ya magoli 2-2 jana usiku.
Katika mchezo wa jana usiku uliopigwa kwenye uwanja wa Bramall Lane ulishuhudia Che Adams akiifungia Sheffield magoli mawili kwenye dakika ya 77 na 79 baada ya Christian Eriksen kuipatia Spurs goli la kuongoza kwenye dakika ya 28 ya mchezo huo.
Lakini wakati mpira ukikaribia kumalizika na Sheffield wakiamini wanaingia fainali alikuwa ni Eriksen tena aliyeisawazishia Spurs kwenye dakika ya 88 ya kipindi cha pili na kufanya matokeo kuwa 2-2 na kuzima kelele za mashabiki wa Sheffield na ndoto za kufika Wembley.
Kwa matokeo hayo Spurs imeingia fainali kwa jumla ya magoli 3-2 na hivyo itacheza mchezo wa fainali ya kombe hilo la Capita One kwenye uwanja wa Wembley dhidi ya Chelsea tarehe 1 ya mwezi Machi mwaka huu.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!