Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 January 2015
Tuesday, January 06, 2015

Hatimaye wenyeji wa Afcon watangaza kocha wa timu yao





Na Florence George


Zikiwa zimebakia siku 11 kabla ya michuano ya kombe la mataifa ya Afrika maarufu kama Afcon kuanza ,hatimaye wenyeji wa michuano hiyo nchi ya Equatorial Guinea imemtangaza Esteban Becker kuwa kocha mkuu wa timu hiyo.


Becker amechukua nafasi ya kocha aliyefukuzwa Andoni Goikoetxea ambaye alionyeshwa mlango wa kutokea baada ya kupata matokeo mabovu katika michezo za kujiaandaa na michuano ambapo timu hiyo ilikuwa imeweka kambi katika nchi ya  Ureno hali iliyopelekea waajili wake kuvunja mkataba na kocha huyo.

Kocha Becker, alifanikiwa kuiongoza timu ya taifa ya Wanawake wa Taifa hilo kutwaa ubingwa wa Afrika kwa upande wa Wanawake mwaka 2012,hiyo chama cha mpira nchini humo kinaamini kocha huyo ataweza kuipatia mafanikio timu hiyo kama alivyofanya kwa timu ya Wanawake.

Kocha Becker anatarajiwa kuwa na timu hiyo mapema pindi timu hiyo itakaporejea toka mjini Lisbon nchini Ureno amabapo inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki na nchi ya
Cape Verde siku ya Jumatano wiki hii.




0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!