Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 January 2015
Tuesday, January 06, 2015

Droo ya raundi ya Nne ya kombe la FA yapangwa






Na Florence George

Hatimaye droo ya raundi ya nne ya michuano ya kombe la FA imepangwa hapo jana huku baadhi ya vigogo wa ligi kuu nchini Uingereza wakionekana kupangwa na timu za madaraja ya chini.


Cambridge United ambayo inashiri ligi daraja la nne Nchini Uingereza ndio timu la daraja la chini sana iliyobaki kwenye michuano hiyo itakumbana na mtihani mgumu pale itakapowakiribisha Mabingwa mara 11 wa michuano hiyo timu ya Manchester United.


Mabingwa watetezi wa michuano,timu ya Arsenal watasafiri hadi ligi daraja la pili kucheza na timu ya Brighton & Hove Albion huku vinara wa ligi kuu nchini Uingereza timu ya Chelsea yenyewe watapambana na timu ya Millwall au Bradford City inayoshiriki ligi daraja la tatu kati ya January 24 au 25.

Mabingwa wa Uingereza timu ya Manchester City itakuwa katika dimba la Etihad Stadium kuwakaribisha timu ya Middlesbrough huku West Brom watakuwa wageni wa Birmingham City.

Vijana wa Brendan Rogders timu ya Liverpool ambayo iliwafunga timu ya AFC Wimbledon magoli 2-1 itawakaribisha timu ya Bolton Wanderers,amabayo itamrejesha mchezaji wa zamani wa Liverpool, Emile Heskey katika dimba la Anfield akiwa na jezi ya Bolton. 

Michezo ya raundi ya nne ya kombe hilo inatarajiwa kupigwa kati ya tarehe 24 hadi 25 January .Ratiba kamili ni kama ifuatayo;

Southampton or Ipswich Town (II) v Crystal Palace
Cambridge United (IV) v Manchester United
Blackburn Rovers (II) v Swansea City
Chelsea v Millwall (II) au Bradford City (III)
Derby County (II) v Scunthorpe United (III) au Chesterfield (III)
Preston North End (III) v Sheffield United (III)
Birmingham City (II) v West Bromwich Albion
Aston Villa v AFC Bournemouth (II)
Cardiff City (II) v Reading (II)
Liverpool v Bolton Wanderers (II)
Burnley au Tottenham Hotspur v Leicester City
Brighton & Hove Albion (II) v Arsenal
Rochdale (III) v Stoke City
Sunderland v Fulham (II) au Wolverhampton Wanderers (II)
Doncaster Rovers (III) au Bristol City (III) v Everton au West Ham United
Manchester City v Middlesbrough (II)




0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!