Searching...
Image and video hosting by TinyPic
31 December 2014
Wednesday, December 31, 2014

Yaya Toure apingana na Bosi wake!


Na Chikoti Cico

Kiungo wa timu ya Manchester City, Yaya Toure apingana na kocha wa timu hiyo Manuel Pellegrini kuhusu taarifa za kwamba aliumia kwenye mchezo dhidi ya West Brom na ndiyo maana hakucheza dhidi ya Burnely siku ya Jumapili, mchezo ulioisha kwa sare ya magoli 2-2 na kuifanya City ishindwe kuikaribia Chelsea kileleni.

Baada ya mchezo huo dhidi ya Burnley kocha wa Manchester City Manuel Pellegrini alikaririwa na vyombo vya habari akisema Toure alipata matatizo ya mtoki kwenye mchezo dhidi ya West Brow siku ya “boxing day” na ana hati hati ya kutokucheza mchezo wa mwaka mpya dhidi ya Sunderland.

Lakini usiku wa Jumanne Toure aliandika kwenye ukurasa wake wa tweeter kwamba “taarifa tu kusema bosi alinipumzisha kwenye mchezo wa Burnley, sijaumia, hakika natumai ntahusishwa dhidi ya Sunderland #ComeonCity#.

Wakati akiongea na vyombo vya habari baada ya mchezo dhidi ya Burnley siku ya Jumapili Pellegrini alisema “Yaya Toure hakuweza kucheza leo, ilikuwa ni hatari kwake.

Wachezaji waliocheza leo ndiyo wachezaji ambao waliweza kucheza, Yaya alijiskia tatizo mwanzoni mwa mchezo wa mwisho dhidi ya West Bromwich”.

Na alipoulizwa nafasi ya Yaya kucheza dhidi ya Sunderland Pellegrini alisema “tutaona, tunatumai kwamba atacheza kwasababu lilikuwa tatizo dogo lakini baada ya masaa 48 labda itakuwa hatari zaidi kujirudia, ni jeraha la misuli kwenye mtoki wake”

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!