Na Chikoti Cico
Nahodha na beki mahiri wa timu ya Chelsea John Terry akaribia kufikia rekodi ya beki wa zamani wa Everton David Unsworth ya beki mwenye magoli mengi kwenye ligi kuu nchini Uingereza, Unsworth anashikilia rekodi hiyo akiwa na magoli 38 ambayo sehemu kubwa ya magoli hayo aliyafunga wakati akiichezea timu ya Everton.
John Terry mpaka sasa amefikisha magoli 35 katika michezo aliyoichezea timu ya Chelsea kwenye ligi kuu nchini Uingereza huku akipitwa na Unsworth kwa magoli matatu tu, goli la 35 la Terry alilifunga dhidi ya Stoke City usiku wa Jumatatu katika ushindi wa Chelsea wa magoli 2-0.
Pamoja na kuwa na umri wa miaka 34 Terry ameendelea kuwa nguzo imara kwenye ukuta wa Chelsea na hivyo kuisaidia timu hiyo kuongoza kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 42 huku ushindi dhidi ya Stoke City ukiwa ni wa 13 toka msimu wa mwaka 2014/15 kuanza kwa timu hiyo kutoka London.
Wakati Terry akishikilia nafasi ya pili kwenye listi hiyo ya mabeki wenye magoli mengi kwenye ligi ya Uingereza, Ian Harte anashikilia nafasi ya tatu akiwa na magoli 28 huku beki na mpigaji penati wa Everton Leighton Baines akishikilia nafasi ya nne akiwa na magoli 26, na anayekamilisha “top five” ya mabeki hao bora kwa ufungaji ni beki wa zamani wa Arsenal na Chelsea William Gallas ambaye ana magoli 25.
0 comments:
Post a Comment