Searching...
Image and video hosting by TinyPic
7 December 2014
Sunday, December 07, 2014

PSG yarudi kileleni mwa ligi kuu nchini Ufaransa





Na florence George

klabu ya soka ya Paris Saint-Germain imefanikiwa kukaa kileleni mwa ligi kuu nchini Ufaransa mara baada ya kushinda magoli 2-1 dhidi ya Fc Nantes katika mchezo uliopigwa siku ya jumamosi usiku.

kaika mchezo huo Fc Nantes ndio waliokuwa wa kwanza kupata goli kupitia kwa Alejandro Bedoya kabla ya mchezaji wa kimataifa wa Sweden Zlatan Ibrahimovic kufunga goli la kusawazisha kisha akafunga la pili kwa mpira wa adhabu na kuipatia timu yake pointi zote tatu.

kwa matokeo hayo yameiwezesha PSG kukaa kileleni kwa kufikisha pointi 37 katika michezo 17 iliyocheza msimu huu ,pointi mbili zaidi ya
Olympique de Marseille iliyopo nafasi ya pili yenye pointi 35 katika michezo 16 iliyocheza msimu huu.

Olympique de Marseille itashuka dimbani jumapili kumenyana na Metz mechi ambayo itakuwa na ushindani kwani Marseille watahitaji ushindi ili waweze kurudi kileleni mwa ligi hiyo.

hadi hivi sasa PSG imefanikiwa kucheza michezo 23 bila kufungwa katika michuano mbalimbali barani ulaya iliyocheza msimu huu.

sasa PSG wanaelekeza nguvu zao katika mechi dhidi ya Fc Barcelona siku ya jumatano katika ligi ya mabingwa barani ulaya mechi itakayopigwa katika jimba la Camp Nou.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!