Searching...
Image and video hosting by TinyPic
6 December 2014
Saturday, December 06, 2014

manchester city yaifukuzia chelsea kileleni


 Na florence george

klabu ya soka ya manchester city imeisogelea kwa karibu timu ya soka ya chelsea mara baada ya kuifunga timu ya soka ya everton goli 1-0 mechi iliyochezwa kwenye dimba la etihad stadium.

katika mechi hiyo iliyokuwa na upinzani mkubwa ilishuhudia gori pekee la manchester city likiwekwa kimiani na mchezaji kutoka ivory coast yaya toure kwa mkwaju wa penati katika kipindi cha kwanza gori lililodumu hadi dakika 90 na kuifanya city kufikisha pointi 33 katika michezo15,pointi 3 nyuma ya vinara wa ligi hiyo chelsea yenye pointi 36 mara baada ya kufungwa na newcastle united magori 2-1 katika dimba la st. james park.

hata hivyo mshambuliaji tegemeo wa timu hiyo muargentina sergio aguero hakuweza kuendelea na mchezo huo baada ya kuumia kifundo cha mguu katika dakika ya pili tu ya mchezo huo na nafasi yake kuchukuliwa na kijana mdogo jose pozo.

kuumia kwa mshambuliaji huyo ni pigo kwa manchester city kwani hadi sasa ameshafunga magoli 14 katika mechi 15 za ligi kuu uingereza msimu huu,hivyo kunawasiwasi anaweza kosekana katika mchezo muhimu wa kufuzu ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya as roma wiki ijayo ambayo pia yaya toure hatokuwemo kutokana na kutumikia adhabu yake ya kadi nyekundu,huku pia david silva akiwa bado majeruhi.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!