real madrid haikamatiki nchini hispania
Na florence george
klabu ya soka ya real madrid imezidi kujichimbia kileleni mwa ligi kuu nchini hispania mara baada ya kuifunga klabu ya soka ya celta vigo magoli 3-0 katika mechi iliyochezwa kwenye nyasi za santiago bernabeu.
sasa timu hiyo imefikisha pointi 36 kwenye michezo 14 iliyocheza kwenye ligi hiyo huku ikiwaaacha athletico madrid katika nafasi ya pili ikiwa na pointi 32 ikiwa tayari imecheza michezo 14 pia,huku fc barcelona ikiwa katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 31 katika mechi 13 iliyocheza.
katika mechi hiyo ilishuhudiwa nyota wa timu hiyo cristiano ronaldo akifunga hat trick na kuweka rekodi ya kuwa mchezaji aliyefunga hat trick nyingi katika ligi kuu nchini humo ,ilikuwa ni hat trick yake ya 23 kwenye ligi kuu tangu alipojiunga na miamba hiyo ya hispania mwaka 2009,pia aliweza kufikisha jumla ya magoli 200 katika mechi 178 alizoichezea real madrid katika ligi kuu nchini humo.
kwa ushindi huo sasa real madrid imeshinda michezo 18 mfululizo ,michezo 11 kwenye ligi kuu,na michezo 7 kwenye michuano mingine,sasa real madrid inajiandaa na mchezo wa klabu bingwa ulaya dhidi ya klabu ya ludogrets mchezo utakaochezwa siku ya jumanne usiku.
0 comments:
Post a Comment
Click to see the code!
To insert emoticon you must added at least one space before the code.