Brian Majwega uso kwa uso na ndugu zake.
Na Oscar Oscar Jr
Baada ya hapo jana timu ya Azam kuibuka na ushindi wa bao 3-1 mbele ya timu ya Vipers, jioni ya leo vijana hao wa kocha Joseph Omog watashuka dimbani kupambana na mabingwa watetezi wa ligi kuu nchini Uganda, timu ya KCCA.
Tayari kiungo mshambuliaji wa Azam ambaye amesajiliwa wiki iliyopita Brian Majwega akitokea timu ya KCCA amepangwa kwenye mchezo huo ambapo anakwenda kukutana na timu yake ya zamani kwa mara ya kwanza.
Majwega amesajiliwa na Azam kwa mkataba wa miaka miwili kwa kiasi cha fedha kinachosadikika kuwa ni Dolla za Kimarekani 20,000.
Huu ni mchezo wa nne kwa Azam kushuka dimbani wakiwa katika kambi yao ya siku 10 nchini Uganda huku timu hiyo ikipoteza mechi mbili za awali na kushinda mchezo wao wa tatu.
Mshambuliaji mwenye magoli mengi msimu huu akiwa na wanalamba lamaba hao, Didier Kavumbagu ameanzia benchi kwenye mchezo huo ambao unatarajiwa kuanza majira ya saa 10: 30 Jioni ya leo.
KIKOSI KINACHOANZA LEO
1. AISHI MANULA
2. SHOMARI KAPOMBE
3. ERASTO NYONI
4. AGGREY MORIS
5. PASCAL WAWA
6. MUDATHIR YAHYA
7. HIMIDI MAO
8. SALUM ABUBAKAR
9. GAUDENCE MWAIKIMBA
10. AMRI KIEMBA
11. BRIAN MAJWEGA
AKIBA
1. MWADINI ALI
2. WAZIRI SALUM
3. GADIEL MICHAEL
4. DAVID MWANTIKA
5. ABDALLAH KHERI
6. KHAMISI MCHA
7. FARID MUSSA
8. KELVIN FRIDAY
10. DIDIER KAVUMBAGU
0 comments:
Post a Comment