Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 December 2014
Sunday, December 21, 2014

Borussia Dortmund yapigwa tena ,Bayern Munich Haikamatiki.





Na Florence George


Hali bado si shwari katika timu ya soka ya Borussia Dortmund mara baada ya kufungwa magoli 2-1 na timu ya soka ya Werder Bremen katika muendelezo wa mechi za ligi kuu Nchini Ujerumani mchezo uliopigwa hapo jana.

Mabingwa hao wa Ujerumani wa mwaka 2011na 2012 walijikuta katika wakati mgumu mara baada ya mchezaji wa Werder Bremen, Davie Selke kuifungia timu yake goli la kuongoza katika dakika ya tatu ya mchezo huo,goli hilo lilidumu hadi mapumziko.

Dortmund walijitahidi kutaka kusawazisha goli hilo lakini alikuwa ni Fin Bartels aliyeifungia Werder Bremen goli la pili, kabla ya Mats Hummels kufunga goli la kufutia machozi la Dortmund katika dakika ya 69.

Hiyo ilikuwa ni mechi 10 Dortmund kupoteza katika msimu huu ambapo hadi sasa wanashikiria nafasi ya 17 huku wakiwa na pointi 15 ,pointi mbili nyuma ya VfB Stuttgart iliyo nafasi ya 16 huku wakiombea mabaya timu ya Freiburg ifungwe na Hanover siku ya jumapili ili iendelee kubaki nafasi hiyo ya 17.

Kwa upande mwingine timu ya Bayer Leverkusen ilitua hadi nafasi ya tatu kwa kufikisha pointi 28, shukrani kwa goli la kusawazisha la Karim Bellarabi katika dakika ya 83 liliwasaidia kugawana pointi na timu ya Eintracht Frankfurt.

Borussia Mönchengladbach ilijikuta ikishuka hadi nafasi ya nne ikiwa na pointi 27 ,pointi moja nyuma ya Leverkusen mara baada ya kufungwa magoli 2-1 na timu iliyopo kwenye kiwango cha hali ya juu msimu huu klabu ya Augsburg.

Vinara wa ligi hiyo timu ya Buyern Munich walifanikiwa kuifunga timu ya Mainz 05 magoli 2-1 siku ya Ijumaa Usiku,shukrani kwa goli  la dakika ya 90 la mdachi Arjen Robben hivyo kufikisha pointi 45 ponti 11 zaidi ya timu ya VfL Wolfsburg iliyopo nafasi ya pili ikiwa na pointi 34.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!