Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 December 2014
Sunday, December 21, 2014

Arsenal waweka rekodi jana pale Anfield.


Na Oscar Oscar Jr

Hatimaye mpambano uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na wadau wa soka la ligi kuu nchini Uingereza baina ya Liverpool na Arsenal ulimalizika kwa timu hizo kutoka sare ya kufungana mabao 2-2. 

Magoli ya Arsenal yalifungwa na Olivier Giroud na Methew Debuchy huku yale ya Liverpool yakiwekwa wavuni na Philippe Coutinho na Martin Skrtel.

Kwa mara ya kwanza Arsenal walionekana kupoteza mipira mingi hasa kipindi cha kwanza na mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, Arsenal walikuwa wamemiliki mpira kwa asilia 36.5. 

Hizi ni asilimia chache kuhawi kumilikiwa na Arsenal tangu waanze kucheza ligi kuu msimu huu huku Liverpool wakipata 63.5 hii ni rekodi ya aina yake.

Matokeo hayo yanawapeleka Liverpool hadi kwenye nafasi ya 10 ya msimamo wa ligi kuu baada ya kutimiza alama 22 na wanabakia kuwa nyuma ya West Ham United ambao wanakamata nafasi ya nne kwa pointi tisa zaidi kwani West Ham tayari wanapointi 31 huku Arsenal wakikamata nafasi ya sita.

Mabadiliko aliyofanya kocha Arsene Wenger hasa dakika za mwisho, yaliwafanya Liverpool ambao walikuwa pungufu baaada ya Fabio Borin kuingia na kupewa kadi nyekundu kuongeza uhai na hatimaye kupata bao la kusawazisha huku zikiwa zimesalia dakika mbili za nyongeza.

Arsenal walikuwa wanaongoza kwa bao 2-1 hadi dakika 90 zinamalizika lakini mwamuzi aliongeza dakika tisa baada ya mpira kusimama sana wakati Martin Skrtel alipogongana na Olivier Giroud na kuchanika kichwani na hapo dipo kocha wa Arsenal alipoibomoa timu yake kwa kuwatoa Alexeis Sanchez, Olivier Giroud na Oxlade Chamberlain.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers bado alishindwa kumuamini Rickie Lambert kama mshambuliaji na badala yake akaamua kumpanga kiungo mshambuliaji, Raheeem Sterling kwenye nafasi hiyo ambayo haonekani kama anaitendea haki.

Mfumo wa walinzi watatu huku Henderson na Markovic wakitumiwa kama mabeki washambuliaji wa pembeni, ulionekana kufanya kazi kwa Rodgers na kufanikiwa kuzui mashambulizi ya kushitukiza kutoka kwa vijana wa Arsenal ambao wamekuwa wakinufaika na mbinu hiyo.

Hakuna timu ambayo ilistahili ushindi kwenye mchezo wa jana na kwa matokeo hayo, sokastadium inaona kama yalistahili kwa pande zote mbili. 

Kwa upande wa pili, mchezo wa mapema kati ya Newcastle United dhidi ya Sunderland ulianza kuzua hofu tena kwa kocha Alan Pardew baada ya Newcastle kufungwa bao dakika ya 90 na kuwafanya Sundreland kuondoka na alama zote tatu.

Siku za hivi karibuni, Alan Pardew amekuwa mnyonge sana anapokutana na watani zao timu ya Sunderland ambao wanaongozwa na kocha Gues Poyet. 

Bao pekee la mchezo huo uliofanyika kwenye dimba la St. James' Park lilifungwa na mchezaji wa zamani wa Manchester City, Adam Johnson.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!