Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 December 2014
Sunday, December 21, 2014

Bingwa mtetezi afanya mambo Hispania. Hat-Trick yaunguruma.


Na Oscar Oscar Jr

Bingwa mtetezi wa ligi kuu nchini Hispania, klabu ya Atletico Madrid jana waliweza kufanikiwa kumaliza mwaka kwa ushindi mnono wa bao 4-1 dhidi ya timu ya Athletic Bilbao ugenini. Ushindi huo ulikuja baada ya Athletic Bilbao kutangulia kufunga bao dakika ya 17 tu mchezo.

Mabao matatu yaliyofungwa na Antonie Greizmann na moja la Raul Garcia kwa mkwaju wa penati yalitosha kuwapatia alama tatu vijana wa kocha Diego Semeon. Goli pekee la Athletic Bilbao lilifungwa na Rico Moreno lakini halikutosha kuwapa alama yoyote.

Kwa ushindi huo sasa, Atletico Madrid wanafikisha alama 35 kutokana na mechi 16 na kushika nafasi ya tatu nyuma ya Barcelona amabao wanakamata nafasi ya pili wakiwa na alama 38 na Real Madrid wakisalia kileleni wakiwa na alama 39.

Real Madrid watakuwa na mchezo mmoja pungufu kutokana na wao kushiriki michuano ya kombe la Dunia kwa ngazi ya vilabu iliyomalizika nchini Morocco hivi karibuni kwa mabingwa hao wa Ulaya kushinda taji hilo.

Baada ya kupoteza mchezo huo, klabu ya Athletic Bilbao imejikuta ikisalia kwenye nafasi ya 11 wakibakia na alama 19 pamoja na kuwa wao ndiyo waliotawala mchezo wa jana kwa umiliki wa mpira kwa asilimia 57.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!