Searching...
Image and video hosting by TinyPic
21 December 2014
Sunday, December 21, 2014

Msitegemee makubwa kwa Hans Van Der Pluijm


Na Samuel Samuel
0752415551

Baada ya mechi ya mtani jembe mwaka jana na Simba SC kuibuka kidedea kwa ushindi wa magoli 3-1 maboss wa Yanga walimtupia virago Ernie Brandts na kumleta nchini mzee Hans chini ya usaidizi wa Boniface Mkwasa. 

Baada ya kuifikisha Yanga SC raundi ya pili klabu bingwa Afrika na kuibuka washindi wa pili ndani ya VPL wakiwaacha Azam FC wakibeba ndoo ya VPL wote waliondoka . 

Ikumbuke Yanga chinu ya Hans ilikuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, kasi, na ufungaji mkubwa wa magoli. Timu ilitimia kila idara. Safu ya ulinzi ikiwa na Dida, Twite, Luhende, Canavaro na Yondani. 

Ilikuwa ni moja ya beki ngumu kupenyeka na kikubwa ilisaidia mashambulizi , njoo kati kulikuwa na injini kama Athuman Idd Chuji na Frank Domayo " chumvi" hapo ndipo siri ya ushindi wa timu ya Hans ulipokuwa umejificha hasa alipoanza kumtumia Frank Domayo kama Chief holding mid fielder. 

Hans alijaaliwa kuwa na mshambuliaji mzuri wa kati Didier Kavumbagu ambaye alikuwa na uwezo binafsi kulazimisha ushindi na hata kugeuka play maker mbele ya safu ya ushambuliaji. Ligi inakwisha Didier ana magoli 11 huku kiungo mshambuliaji Mrisho Ngasa naye akiwa ametupia nyavuni magoli 13 sitaki kukumbuka utamu wa kazi ya Hamisi Kiiza ambaye naye alitaradadi vya kutosha na alikuwa na magoli 12. 

Anakumbukwa zaidi kwenye mechi zote dhidi ya Kagera Sugar kule Kaitaba na jijini Dar kwa magoli yake muhimu ya ushindi. Pia Hans alimtumia Emmanuel Okwi kwenye zaidi ya mechi nne na kiungo huyo wa pembeni aliing'arisha klabu hiyo vizuri akikumbukwa zaidi kwa goli lake la kufutia machozi ndani ya mtani jembe. 

Yanga ile ukijiuliza kwa nini ilikosa ubingwa unaweza inama chini na kuanza kulia. Sasa Hans na Mkwasa wake wamerudi tena Jangwani kwa dhana ile ile ya kuikomboa Yanga kimataifa kwa ligi ya shirikisho na kulichukua kombe la VPL lililopo Chamazi. Je watafanikiwa safari hii? 

Yanga hii ina changamoto nyingi sana kuliko waliyoikuta na waliyoiacha. Hans alikuwa na vipuri kama Frank Domayo ambaye katimkia Azam FC sambamba na Didier Kavumbagu . Chuji, Luhende , Kiiza wote wametupiwa virago huku Emanuel Okwi akijiunga na Simba SC. Kule mbele si Ngasa yule aliyeibuka mfungaji bora Afrika kwa mechi mbili tu dhidi ya Komorozone achilia mbali magoli 13 ndani ya ligi lakini hivi sasa hata goli la off side katika mechi saba alizocheza. 

Hans anakutana na Yanga ambayo haina playing partnerships kwa sasa. Huoni ule muunganiko wa kushambulia uliokuwa unaanzia kwa Domayo , Niyonzima , Kavumbagu, Ngasa na Hamisi Kiiza. 

Hans anakutana na forward line yenye watu wenye umri kidogo kama Dany Mrwanda (31) , Hamisi Tambwe (30) wakisaidiana na Kpah Sherman . 

Hans ni muumini wa soka la kasi na kutumia nguvu nyingi pande zote ( equal energy) . Wataweza? Kiungo cha kati baada ya kutimuliwa Emerson bado haieleweki ni nani Hans atamtumia kati ya Twite ambaye yeye humuhusudu kama beki wa pembeni na Salumu Telela . Yetu macho. 

Tunasubiri kuona kama Ngasa atarudia makali yake na Yanga kubeba kombe. Ukiitazama Yanga kiufundi ni kama Hans na Mkwasa wanaanza MOJA.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!