Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 November 2014
Friday, November 28, 2014

Uchambuzi: Liverpool vs Stoke City


Na Chikoti Cico

Timu ya Liverpool ambayo imekuwa na matokeo mabovu kwenye michuano mbalimbali, itaikaribisha Stoke City kwenye uwanja wao wa Anfield katika kutafuta alama tatu muhimu kwenye mfululizo wa mechi za ligi kuu nchini Uingereza.

Kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers anatarajia kuingia kwenye mchezo huo akiendelea kuwakosa washambuliaji wake Mario Balotelli na Daniel Sturridge hivyo Rickie Lambert, ambaye katika mechi mbili zilizopita amefunga magoli mawili akitarajiwa kuongoza safu ya ushambuliaji ya timu hiyo kwenye mchezo dhidi ya Stoke City.

Liverpool ambayo mpaka sasa inashika nafasi ya 12 ikiwa na alama 14 kwenye msimamo wa ligi, wanaingia kwenye mchezo huo huku wakiwa wamepoteza michezo minne kati ya mitano katika mashindano mbalimbali matokeo ambayo yanafanya ushindi dhidi ya Stoke City kuwa kitu cha muhimu kwa Liverpool.

Takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa Liverpool, Rickie Lambert ameifunga Stoke mara tatu katika mechi nne alizocheza dhidi yao huku mshambuliaji mwingine wa Liverpool, Mario Balotelli akishindwa kuziona nyavu kwa masaa 12 na dakika 48 katika mechi alizoichezea Liverpool.

Kikosi cha Liverpool kinaweza kuwa hivi: Mignolet; Johnson, Skrtel, Toure, Moreno; Gerrard; Henderson, Allen; Lallana; Sterling, Lambert.

Kwa upande wa kocha wa Stoke City, Mark Hughes ataingia kwenye mchezo huo huku akiwakosa Victor Mosses ambaye atakuwa nje kwa muda wa wiki sita mpaka nane, Robert Huth, Peter Odemwingine na Dio natan Teixeira ambao ni majeruhi.

Stoke mpaka sasa wanashika nafasi ya 11 kwenye msimamo wa ligi wakiwa na alama 15 huku wakipishana na Liverpool kwa alama moja tu kitu kinachoifanya mechi hiyo kuwa ya piga nikupige katika kutafuta alama tatu muhimu.

Wakati huo huo, takwimu zinaonyesha Stoke hawajashinda mchezo hata mmoja katika michezo 29 iliyopita waliyocheza na Liverpool Anfield.

Wametoka sare michezo minne na kufungwa michezo 25 pia takwimu pia zinaonyesha mshambualiaji wa Stoke City, Jonathan Walters amefunga magoli manne katika mechi sita alizocheza dhidi ya Liverpool.

Kikosi cha Stoke City kinaweza kuwa hivi: Begovic; Bardsley, Shawcross, Wilson, Muniesa; Sidwell, N'Zonzi; Walters, Bojan, Diouf; Crouch

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!