Searching...
Image and video hosting by TinyPic
28 November 2014
Friday, November 28, 2014

Uchambuzi: Manchester United vs Hull City


Na Chikoti Cico

Mchezo mwingine wa ligi kuu nchini Uingereza, utakuwa kati ya Manchester United dhidi ya Hull City mchezo utakaopigwa kwenye uwanja wa Old Trafford huku United wakitafuta alama tatu ili kuendelea kubaki kwenye nafasi nne za juu (top four) na Hull City wakitaka kuondoka kwenye hatari ya kushuka daraja.

Manchester United wataingia kwenye mchezo kutafuta alama tatu muhimu ili kuendelea kujikita kwenye nafasi nne za juu na kuendela kupunguza tofauti ya alama 13 dhidi ya vinara Chelsea.

Pamoja na hayo United watawakosa Daley Blind, Rafael, Luke Shaw, Phil Jones na Jonny Evans ambao ni majeruhi huku kukiwa na taarifa ya uwezekano wa Rojo na Falcao kucheza mchezo huo dhidi ya Sunderland.

United inayofundishwa na Mdachi, Luis Van Gaal inashika nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi ikiwa na alama 19 baada ya kushinda mchezo uliopita dhidi ya Arsenal kwa magoli 2-1, huku ukiwa ni ushindi wa kwanza ugenini kwa kocha huyo.

Takwimu zinaonyesha nahodha wa United Wayne Rooney amefunga magoli sita katika mechi nne alizocheza na Hull City huku Manchester United ikishinda mechi tisa iliyopita dhidi ya Hull City katika michuano mbalimbali.

Kikosi cha Manchester United kinaweza kuwa hivi: De Gea; McNair, Smalling, Blackett; Valencia, Carrick, Fellaini, Young; Di Maria; Rooney, Van Persie

Kwa upande wa Hull City, kocha wa timu hiyo Steve Bruce atawakosa Gaston Ramirez anayetumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyopewa kwenye mchezo dhidi ya Spurs na mshambuliaji Abel Hernandez aliyerejea nyumbani Uruguay ambako mkewe anatarajiwa kujifungua.

Huku wakishika nafasi ya 17 wakiwa na alama 11 kwenye msimamo wa ligi, timu ya Hull City inatarajia kuingia kwenye mchezo huo kupigana kufa na kupona kutafuta alama tatu muhimu ili kuondokana na hatari ya kushuka daraja.

Ingawa timu hiyo imekuwa na rekodi mbaya ugenini kwani katika michezo 11 iliyopita, imeshinda mchezo mmoja tu na kufungwa michezo sita na kutoka sare michezo minne.

Takwimu pia zinaonyesha katika michezo 11 ya ugenini kwa Manchester United, Hull city imefungwa michezo 10 na kutoka sare mchezo mmoja.

Kikosi cha Hull City kinaweza kuwa hivi: Harper; Chester, Dawson, Davies; Elmohamady, Huddlestone, Livermore, Diame, Robertson; Ben Arfa, Jelavic.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!