Na Chikoti Cico.
Timu
ya Real Madrid yaweka rekodi ya kushinda michezo 16 mfululizo. Michezo
hiyo inajumuisha michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya na ligi kuu nchini
Hispania maarufu kama la liga. Hii ikiwa ni kwa mara ya kwanza kwenye
historia ya klabu hiyo.
Madrid ambao wanaongoza kwenye msimamo wa la liga wakiwa na alama 33 baada ya michezo 13, walikamilisha rekodi hiyo usiku wa jumamosi katika mechi dhidi ya Malaga ambayo walishinda kwa magoli 2-1.
Magoli ya Madrid yalifungwa na Karim Benzema na Gareth Bale kabla ya Santa Cruz kuipatia Malaga goli la kufutia machozi.
Timu hiyo inayofundishwa na kocha Carlo Ancelotti, inaweza kuendeleza rekodi hiyo ya ushindi wimbi kwani inatarajiwa kucheza mechi tatu kwenye uwanja wake wa nyumbani Santiago Bernabeu.
Watacheza dhidi ya timu ya Cornella kwenye kombe la Mfalme (Copa del Rey), Celta Vigo kwenye la liga na Ludogorets kwenye mechi ya ligi ya mabingwa Ulaya.
Kwa rekodi hiyo ya ushindi wa mechi 16 mfululizo kocha Ancelotti amevunja rekodi iliyowekwa na makocha wa zamani wa Madrid Miguel Munoz mwaka 1960-1961 na Jose Mourinho mwaka 2011-2012 ambao waliweka rekodi ya ushindi wa michezo 15 mfululizo kila mmoja.

0 comments:
Post a Comment