MWANASHERIA wa nyota wa Simba Emmanuel Okwi, Edgar Aggaba (pichani) ametua nchini kimya kimya na kuweka wazi kwamba mchezaji huyo amebakiza mwezi mmoja Msimbazi huku akitoa masharti mapya ya usajili ambayo hayatofautiani na yale ya kiungo Jonas Mkude aliyesaini Msimbazi hivi karibuni.
Akizungumza na Mwanaspoti alisema Simba wanatakiwa kumuandalia Okwi dau zuri la usajili lisilopungua Dola 30,000 (Sh 52.2 ml), mshahara mzuri, nyumba na gari ya kisasa ya kutembelea vitu ambavyo wanatakiwa kuvikamilisha kabla ya kusaini mkataba mpya.
“Sikuja kwa ajili ya Simba ndiyo maana hakuna
aliyejua kuwa nipo hapa, Okwi yupo katika kumalizia muda wake wa mkataba
mfupi lakini wakati wowote tunaweza kuanza mazungumzo ya kusaini
mkataba mpya na Simba,”alisema Aggaba.
“Tunataka hayo tunayoyataka yakamilishwe mapema
tena kabla ya mchezaji hajasaini mkataba mpya endapo tutakubaliana,
unajua hata sasa walitakiwa kumpa nyumba na gari lakini Okwi ameniambia
kwamba hajapewa hata nyumba na alikuwa anakaa katika nyumba ya rafiki
yake.”
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo
0 comments:
Post a Comment