Searching...
Image and video hosting by TinyPic
30 November 2014
Sunday, November 30, 2014

Pellegrini asema mbio za kutetea Ubingwa zimerudi kwa City.


Na Oscar Oscar Jr

Baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-0 dhidi ya timu ya Southampton, kocha wa Manchester City, Manuel Pellegrini ameibuka na kusema kuwa, ushindi huo umefufua matumaini ya timu yake kutetea ubingwa. 

Southampton ambao kabla ya mchezo huo walikuwa nafasi ya pili kwenye msimamo, walijikuta wakipokea kichapo cha kwanza wakiwa uwanja wao wa nyumbani na bingwa mtetezi.

Manchester City mara yao ya mwisho kupata ushindi nyumbani kwa Southampton ilikuwa mwaka 2003 ambapo walipata magoli kupitia kwa Robbie Fowler na Paulo Wanchopelakini jana, Kiungo Frank Lampard na Yaya Toure walifunga kila mmoja bao moja huku lingine likifungwa na beki Gael Clichy.

Kompany aliumia katika mchezo huo huku Eliaquem Mangala akipewa kadi nyekundu huku zikiwa zimesalia dakika 17 mchezo umalizike. 

Pellegrini ambaye timu yake itashuka dimbani siku ya jumatano dhidi ya Sunderland, amesema kuwa anatamtumia Martín Demichelis na Dedryck Boyata kama walinzi wa kati, huku pia akionyesha uwezekano wa kumtumia Bacary Sagna kwenye nafasi hiyo.

Ushindi wa City umewafikisha kwenye nafasi ya pili baada ya kutimiza pointi 27 huku Chelsea, wakisalia kileleni wakiwa na pointi ya 32. Southampton wanasalia kwenye nafsi kwenye nfasi ya pili wakiwa na alama 26 na mechi ijayo wanakabiliana na vijana wa Arsene Wenger, timu ya Arsenal.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!