Falcao kutafuata timu kubwa msimu ujao
Na Florence George
Mshambuliaji wa kimataifa wa Colombia Radamel Falcao ambaye anachezea kwa mkopo hadi mwisho mwa msimu huu katika klabu ya Manchester United akitokea Monaco ya nchini Ufaransa hadi ameiweka njia panda timu hiyo kama ataendelea kuichezea timu hiyo msimu ujao.
Falcao aliachwa katika kikosi cha United kilichocheza siku ya jumapili na kuambulia kipigo cha goli 1-0 kutoka kwa Southampton katika dimba la Old Trafford.
Wakala wa mchezaji huyo Jorge Mendes ameviambia vyombo vya habri za Uingereza kuwa anaamini kuwa mchezaji huyo atatafuta timu nyingine kubwa kama kocha Van Gaal hatompa mkataba wa moja kwa moja katika timu hiyo.
Mendes aliendelea kusema kuwa hajui mchezaji huyo ataelekea wapi lakini alisisitiza kuwa Falcao ni mchezaji mzuri na mwenye uwezo mkubwa huku akiamini kuwa mchezaji huyo anauwezo wa kucheza dakika zote 90 uwanjani timu yoyote ile na mechi yoyote ile.
Alimalizia kwa kusema kuwa kwa sasa hajui mchezaji huyo ataelekea wapi laknini anaamini atapata timu kubwa msimu ujao kama ataendelea kubaki Manchester United au la.
Falcao amefanikiwa kufunga magoli matatau katika michezo 12 alizoichezea timu hiyo huku akianza katika michezo saba tu.
0 comments:
Post a Comment