Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 November 2014
Sunday, November 16, 2014

Pelle hatimaye atoka Hospitali.



Mkongwe na nguli wa soka wa Brazil, Pele aliruhusiwa kuondoka hospitali katika mji wa Sao Paulo alikokuwa amelazwa siku ya Jumamosi baada ya madaktari kuona kuwa, hali yake inazidi kuimarika. 

Mkongwa huyo ambaye ana umri wa mika 74, anasumbuliwa na tatizo la figo. Pele, alilazwa hospitali ya Albert Einstein siku ya Jumatano akiwa na maumivu ya tumbo yaliyomlazimu kutohudhuria hafla ya kutoa uzinduzi wa kitabu iliyofanyika kwenye mji wa Santos, anakoishi.

Uchunguzu ilibaina matatizo ya Figo ambayo yalipelekea njia ya haja ndogo kumsumbua. Fundi huyo huyo ambaye anayejulikana sana kama “Mfalme wa Soka” nchini Brazil anatambuliwa kama mmoja wa wachezaji bora zaidi wa soka kuwahi kuishi. 

Amewahi kutangazwa kama Mchezaji Bora wa Karne na shirikisho linalosimamia soka duniani Fifa. Pelle., alicheza katika fainali nne za Kombe la Dunia na kusaidia Brazil kushinda taji hilo la dunia mara tatu, mara ya mwisho ikiwa Mexico 1970.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!