Searching...
Image and video hosting by TinyPic
16 November 2014
Sunday, November 16, 2014

Kocha wa Ujerumani anunua "kesi" ya Podolski



Na Oscar Oscar Jr

Kocha wa timu ya taifa ya Ujerumani, Joachim Loew ameamua kuzungumzia kiwango cha mchezaji wa taifa hilo ambaye anakipiga na klabu ya Arsena, Lukas Podolski.

Loew amekaririwa akisema kuwa, muda mwafaka wa mchezaji huyo kuondoka kwenye klabu hiyo ya Jijini London, Uingereza umewaidia kama mchezaji huyo ana ndoto za kuendelea kucheza mechi za kimataifa.

Kocha huyo amezungumza mara baada ya kuona kiwango cha mshambuliaji huyo ambaye amecheza mechi 121 za timu ya Taifa na kufunga mabao 47, huku kwa sasa akionekana kushuka kiwango kutokana na kusugua benchi kwenye klabu yake.


Loew alimpa Podolski nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha Ujerumani pale walipoilaza timu ya Gibraltar 4-0 siku ya Ijumaa mechi ya kufuzu kwa Euro 2016, lakini mshambuliaji huyo alishindwa kung’aa. 

Baada ya kufunga mabao 47 katika mechi 121 za kimataifa alizocheza, ni majagina wa kitaifa Miroslav Klose na Lothar Matthaeus ambao wamechezea Ujerumani mechi zaidi kumshinda.


Straika huyo wa zamani wa klabu ya Bayern Munich na Cologne bado hajaondoa matumaini ya kurejea kwenye ligi ya Bundesliga pamoja na kuwa, kuna timu nyingi nje ya Ujerumani zinazomtaka.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!