Na Oscar Oscar Jr
Hatimaye timu ya Taifa ya Uholanzi usiku wa leo, imefanya maangamizi mbele ya timu ya Latvia kwa kuichapa mabao 6-0 huku rekodi mbalimbali zikiwekwa na wachezaji wa kidachi.
Nahodha wa timu hiyo, Roben Van Persie ameendelea kujichimbia juu kama mfungaji bora wa muda wote wa Uholanzi baada ya goli lake la leo kufikisha idadi ya mabao 49 kwenye michezo 96.
Habari njema katika mchezo huu ilikuwa kwa mshambuliaji Klaas Juan Huntelaar ambaye alifunga mabao mawili na kumfanya amshushe mkongwa wa klabu ya Arsenal, Dennis Bergkamp ambaye alikuwa anashikilia rekodi ya kuwa mfungaji bora wa Uholanzi kwenye nafasi ya tatu huku akiwa amefunga mabao 37 kwenye mechi 79.
Huntelaar sasa ametinga kwenye nafasi ya tatu baada ya kufikisha magoli 38 katika michezo 68. Wachezaji wengine ambao walifunga magoli mengi wakiwa na timu ya taifa ya Uholanzi ni Patrick Kluivert ambaye anashika nafasi ya pili kwa kuwa na magoli 40 katika mechi 79 ingawa alistaafu soka tangu mwaka 2004.
Wengine ni mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na Real Madrid, Ruud Van Nestelreey alifunga magoli 35 katika mechi 70 na mkongwa wa Kidachi, Johan Cruyff akifnga mabao 33 kwenye mechi 48 na kustaafu soka mwaka 1977.
Kwa magoli hayo sasa, Roben Van Persie anaendelea kuongoza kwa magoli yake 49, huku akifuatiwa na Patrick Kluivert mwenye magoli 40 na Klaas Juan Huntelaar akishika nafasi ya tatu kwa kufikisha magoli 38.
0 comments:
Post a Comment