Taarifa ya Pelle kupelekwa Wodi ya ICU
Na Oscar Oscar Jr
Kongwe wa Brazil, Pelle amekuwa akisumbuliwa na tatizo la matatizo ya njia ya haja ndogo kitu kilichopelekea kulazwa Hospitali katika Jiji la Sao Paulo. Baada ya taarifa hizo kutoka siku ya jumatatu, kumekuwa na ripoti nyingi zinazozungumzia hali yake.
Hivi karibuni mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 74, aliripotiwa kuhamishiwa kwenye Wodi ya ICU kitu ambacho kiliongeza mshituko kwa wadau wa soka ambao wamekuwa wakifuatilia hali ya mkongwe huyo.
Mshauri wa Pelle, Jose Fornos Rodrigues ameamua kuzungumza na kuwatoa watu wasi wasi kwa kusema kuwa, ni kweli Pelle amehamishiwa kwenye Wodi ya ICU na sababu ni kwamba, alikuwa anatembelewa na watu wengi sana hivyo wakaomba apelekwe ICU ili apate muda wa kupumzika.
Mshauri huyo alisisitiza kuwa, hali ya Pelle ni nzuri na anaweza kuruhusiwa leo ili kurudi nyumbani na kuendelea na mambo mengine.
Pelle amekuwa akisumbuliwa na matatizo ya afya yake mara kwa mara siku za hivi karibuni na mtandao huu unatumia fursa hii kumtakia afya njema.
0 comments:
Post a Comment