Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 November 2014
Saturday, November 29, 2014

Pauni milioni 115 zaliwa na mawakala Uingereza.


Na Chikoti Cico

Klabu za ligi kuu nchini Uingereza zimetumia jumla ya kiasi cha pauni milioni 115 kwa mawakala mbalimbali wakati wa usajili kwa vipindi vya viwili vya usajili vilivyopita nchini humo.

Timu ya Chelsea ndiyo inayoongoza katika matumizi ya fedha hizo kwa mawakala mbali mbali ili kukamilisha usajili wa wachezaji kutokea katika madirisha mawili ya usajili yaliyopita.

 Chelsea ilitumia kiasi cha pauni 16,771,328 ikifuatiwa na Liverpool waliotumia kiasi cha pauni 14,308,444 huku Manchester City wakitumia kiasi cha paundi 12,811,946 na Tottenham pauni 10,983,011.

Katika kuonyesha ni jinsi gani timu za Chelsea, Liverpool, Manchester City na Tottenham pekee zimetumia fedha nyingi kwaajili ya mawakala kwa mwaka uliopita, jumla ya fedha hizo ni zaidi ya matumizi ya mishahara ya timu zote kwenye ligi daraja la pili nchini Uingereza.

Timu ambazo zimelipa kiasi kidogo cha fedha kwaajili ya mawakala ni Burnley waliolipa kiasi cha £711,024, Leicester City £1,608,418. Crystal Palace, Hull, Aston VIlla na Southampton ambao wote wamelipa chini ya pauni milioni 3.

Taarifa hii ya ulipaji wa mawakala kwa timu za ligi kuu nchini Uingereza toka Octoba 1 2013 mpaka Septemba 30 2014 inajumuisha pia malipo yaliyofanywa na klabu mbalimbali kwa niaba ya wachezaji ili kukamilisha usajili wa wachezaji hao kwa wakati.

Wakati huo huo, wakala wa mchezaji Mangala aliyesajiliwa kutoka Manchester City Jorge Mendez amekuwa kinara kwa kuingiza faida kubwa kuliko mawakala wengine kutoka timu mbalimbali.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!