Searching...
Image and video hosting by TinyPic
29 November 2014
Saturday, November 29, 2014

Kueleke Malaga vs Real Madrid usiku wa leo.


 Na Oscar Oscar Jr

Wakiwa na alama 30 kutokana na kushuka dimbani mara 12, Real Madrid leo watakuwa ugenini kwenye mchezo wa ligi kuu Hispania pale watakapoumana na timu ya Malaga ambao wanakamata nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi hiyo.

Cristiano Ronaldo ambaye anaongoza kwa upachikaji wa magoli kwenye ligi hiyo mpaka sasa akiwa na mabao 20, anatarajia kuiogoza safu ya ushambuliaji ya kocha Carlo Ancelotti kwenye mchezo huo utakaoanza majira ya saa 4:00 Usiku kwa saa za huku kwetu.

Malaga ambao wanapointi 21, watakuwa nyumbani kuhakikisha kuwa wanapata ushindi na kujivuta kuelekea Top Four ambayo inaonekana kukamatwa na timu za Real Madrid, Barcelona, Atletico Madrid na Valencia.

Ushindi wa leo kwa Real Madrid itakuwa ni rekodi kwani mnamo miaka ya 1960, aliyekuwa kocha wa timu hiyo, Miguel Munoz, Los Blancos walifanikiwa kushinda mechi 15 mfululizo na kipindi cha kocha Jose Mourinho, walifanikiwa kufanya hivyo.

Ushindi wa bao 1-0 walioupata mbele ya Basel kwenye michuano ya klabu bingwa Ulaya, umemfanya kocha Carlo Ancelotti kuifikia rekodi hiyo iliyowekwa na makocha hao wa zamani wa timu hiyo. 

Kama Real Madrid watashinda, huu utakuwa ushindi wao wa 16 mfululizo baada ya kula vichapo mwanzoni mwa ligi kutoka kwa Real Sociedad na Atletico Madrid.

 

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!