KIUNGO Emerson Roque raia wa Brazil amepewa jezi namba 19 katika kikosi cha Yanga ambayo ilikuwa ikitumiwa na kipa chipukizi Yussuf Abdul.
Emerson anafanya mazoezi na kikosi cha kwanza cha Yanga na anatazamwa na benchi lote la ufundi na uongozi ili kama akiwa fiti aweze kusajiliwa kuchukua nafasi ya Geilson Santos ‘Jaja’ ambaye amejiondoa kikosini.
Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh aliliambia
Mwanaspoti kuwa, Emerson amepewa jezi hiyo namba 19 ambayo awali ilikuwa
ikitumiwa na kipa chipukizi Abdul ambaye sasa amejiunga na African
Sports ya Tanga inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza.
“Unajua hii jezi ilibaki bila mtu kwa maana huyu
kipa aliachwa ndiyo akajiunga na African Sports, sasa Emerson alipofika
tukaona bora tumpe kwanza jezi hii halafu kama akitaka kubadili tutajua
baadaye baada ya mambo yake kuwa mazuri,” alisema Hafidh.
Endapo Emerson atalivutia benchi la ufundi la
Yanga, atakutanishwa na viongozi ili waweze kukubaliana kuhusu usajili
na kuna uwezekano mkubwa akasaini mkataba wa miaka miwili.
Katika hatua nyingine, kocha wa Mgambo JKT, Bakari Shime amewashangaa makocha wanaofanya usajili wa mbwembwe huku timu zao zikiwa zimecheza mechi saba.
Badala ya kufanya usajili, Shime aliamua
kuwapumzisha wachezaji wake kwa siku kumi tu kisha akawaita kazini huku
akisisitiza hana haja ya kufanya usajili wowote labda kuziba nafasi kwa
watakaoondoka.
Mgambo ambayo ipo nafasi ya tisa ikiwa na pointi
tisa na ilicheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Yanga na kufungwa mabao
2-0 ndipo Ligi Kuu Bara ikasimama kupisha dirisha dogo la usajili na
michuano mingine ifanyike.
Shime aliliambia Mwanaspoti; “Labda kitokee kitu
kingine lakini sina mpango wa kufanya usajili wowote kwani mechi saba
sidhani kama zinatosha kuweza kujua kama mchezaji fulani hana uwezo au
anao. Niliwapa mapumziko ya siku kumi tu na sasa tupo mazoezini.
“Ninachofanya sasa ni kutazama wale waliochemka na kuwapa mafunzo ili wafanye vizuri katika mechi zijazo, sasa hawa wenzangu wanaofanya usajili sijui tathmini yao wameifanya vipi katika mechi saba tu kati ya 26 ambazo timu inatakiwa ichezea kwa msimu mzima?
“Ninachofanya sasa ni kutazama wale waliochemka na kuwapa mafunzo ili wafanye vizuri katika mechi zijazo, sasa hawa wenzangu wanaofanya usajili sijui tathmini yao wameifanya vipi katika mechi saba tu kati ya 26 ambazo timu inatakiwa ichezea kwa msimu mzima?
“Labda angalau tungekuwa tumecheza hata mechi 13 kama ilivyo kawaida, lakini sijui wenzangu wametumia kigezo gani.”
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo
Source: Gazeti la Mwanaspoti la leo
0 comments:
Post a Comment