Searching...
Image and video hosting by TinyPic
10 November 2014
Monday, November 10, 2014

Hazard awatosa Real Madrid.


Na Chikoti Cico

Mchezaji wa Chelsea na timu ya taifa ya Ubelgiji, Eden Hazard amepinga habari zilizozagaa kwenye vyombo vya kwamba anataka kwenda Real Madrid. Taarifa zilizotoka nchini Hispania wiki iliyopita zilimuhusisha Hazard kutakiwa na Madrid huku timu hiyo ikisemekana kuwa, tayari kumwachia Gareth Bale ili kupata fedha za kumsajili Hazard.

Hazard ambaye mpaka sasa ameifungia timu ya Chelsea magoli matano toka kuanza kwa msimu wa mwaka 2014/2015 huku akiisaidia timu hiyo kuongoza ligi kuu nchini Uingereza, amesema hana nia ya kuihama Chelsea na kwenda kujiunga na Real Madrid.

Akiongea na Canal+ Hazard alisema “ sikuwahi kusema kwamba kama nikiondoka Chelsea itakuwa ni kwa ajili ya Real Madrid, klabu pekee inayonifanya mimi kuota ni Chelsea"

"Nilifanya chaguo kujiunga na Chelsea kwasababu nIlikuwa najua ntakuja kucheza. Huu ni mwaka wangu wa tatu hapa, sijui kama mimi ni hazina kuu ya timu ila nafurahia kwa kucheza kwenye timu hii”

Hazard ambaye alijiunga na Chelsea mwaka 2012 na kushinda tuzo ya mchezaji bora mdogo kwa msimu uliopita wa ligi akiiongelea timu ya PSG na ligi ya Ufaransa maarufu kama “Ligue 1” alisema

“sina majuto nikiangalia Ligue 1, nafikiri kuhusu yajayo na sio yaliyopita. Paris (Saint-German) wana wachezaji wazuri ila Chelsea ina uzoefu na wacheza zaidi kwenye nafasi flani na tuna uzoefu mzuri kwenye ligi ya mabingwa Ulaya.

Hazard aliyesajiliwa na Chelsea toka Lille ya Ufaransa amekuwa akihusishwa na timu mbalimbali kutaka kumsajili hasa baada ya kuendelea kufanya vizuri kwenye ligi kuu ya nchini Uingereza pamoja na ligi ya mabingwa Ulaya.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!