Swansea yashinda rufaa yao
Na Rossa Kabwine
Timu ya Swansea City imeshinda rufaa yao dhidi ya kadi nyekundu ya beki Federico Fernandez, aliyoipata kwenye mchezo wao dhidi ya Liverpool, katika mchezo wa kombe la Capital one.
Katika mchezo huo, Liverpool ilishinda kwa magoli 2-1 na kufanikiwa kuingia katika hatua ya robo fainali ya kombe hilo. Fernandez mwenye miaka 25, alitolewa nje kwa kadi nyekundu baada kumchezea rafu kiungo wa Liverpool Phelippe Coutinho.
Mchezaji huyo wa Argentina, angekosa mechi tatu kama adhabu ya rafu mbaya aliyoicheza. Lakini Swansea walikata rufaa dhidi ya maamuzi ya mwamuzi Keith Stroud na wameshinda.
Beki huyo sasa atakuwepo wikendi hii katika mchezo wa ligi kuu ya Uingrreza ambapo Swansea City watakutana na timu ya Everton. “haikuwa kadi nyekundu kabisa “ alisema kocha wa Swansea Garry Monk.
Baada ya mechi ile, Monk alikutana na mkuu wa waamuzi, Mike Riley siku ya ijumaa ili kujadiliana kuhusu maamuzi mabaya yaliyopeleke timu yake kutolewa katika shindano hilo.
Baada ya Swansea kufungwa 2-1 dhidi ya Stoke City katika ligi kuu ya Uingereza tarehe 19/10/2014, kocha Gary Monk alimshutumu kiungo mshambuliaji wa Stoke City, victor Mosess kwa kudanganya ili apate penati.
Kocha huyo anaunganisha matukio ya Victor Moses na yale yaliyotokea kwenye Capital One Cup dhidi ya Liverpool, na kuamini kabisa kuwa timu yake haitendewi haki na waamuzi.
Fernandez alipewa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya mwamuzi kuona mshambuliaji wa Liverpool, Philippe Coutinho kachezewa rafu mbaya. Swansea City yenye points 14 itakutana na Everton yenye points 12 katika ligi ya uingerza jumamosi hii.
0 comments:
Post a Comment