Said Bahanuz kuondoka Morogoro Kesho.
Na Oscar Oscar Jr
Timu ya Polis Morogoro kesho inajiandaa kuanza safari yake kuelekea mkoani Mtwara kwa ajili ya mchezo wao wa mzungunguko wa 10 ambapo watashuka dimba Nangwanda Sijaona kupambana na timu ya Ndanda fc.
Ndanda Fc mechi yao ya mzunguko wa tisa wakiwa mkoani Mbeya, waliweza kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons huku Polis Morogoro wao wakibanwa mbavu na Stand United nyumbani kwa sare ya bila kufungana.
Akizungumza na SOKA STADIUM, meneja wa timu ya Polis, Manfredy Lwambano amesema kuwa timu hiyo inajiandaa kuondoka Morogoro kesho kuelekea Mtwara na hakuna majeruhi yoyote na kwa maana hiyo watakwenda na kikosi kilichokamilika.
"Tunatarajia kuanza safari yetu kuelekea Mtwara hapo kesho ila kwa sasa bado tupo Morogoro na hatuna majeruhi hata mmoja hivyo tutasafiri na kikosi cha wachezaji wote" Alisema Meneja huyo.
Polis Moro wanashika nafasi ya tano kwenye msimamo wa ligi kuu wakiwa na alama 13 ambazo ni sawa na JKT Ruvu lakini wao wanauiano mzuri wa magoli ya kufungwa na kufunga.
Mshambuliaji Said Bahanuzi ambaye yupo kwenye klabu hiyo kwa mkopo akitokea klabu ya Yanga, bado hajapata bao hata moja licha ya kuonyesha kiwango kizuri kwenye mechi mbili alizocheza na kikosi hicho.
Akizungumzia jambo hilo, Lwambano anasema "Bahanuzi ni mchezaji mzuri na alifunga bao zuri tu dhidi ya Stand United japo mwamuzi alilikataa na uwepo wake ni mchango mkubwa sana kwenye kikosi chetu"
Mchezaji huyo ambaye baada ya kuibuka mfungaji bora wa michuano ya Kagame mwaka 2012, ameonekana kiwango chake kupanda na kushuka kiasi cha timu ya Yanga kushindwa kumpa nafasi na kuamua kwenda kwa mkopo Polis Moro.
Bahanuzi ni moja kati ya wachezaji watakao ondoka Morogoro kuelekea Mtwara kuwakabili Ndanda Fc mchezo utakaopigwa January 10.
0 comments:
Post a Comment