Mbwa avamia uwanja na kumng'ata mchezaji
Na Oscar Oscar Jr
Katika hali isiyo ya kawaida, Mbwa alivamia uwanja wakati wa mchezo wa kombe la ligi nchini Brazili kati ya timu ya Sao Paulo dhidi ya Farroupilha.
Wakati mchezo huo ukiendelea huku timu ya Sao Paulo ikiwa nyuma kwa bao 2-1, mbwa alivamia uwanja na kusababisha mwamuzi wa mchezo asimamishe mpambano.
Mshambuliaji wa Sao Pauolo aliyejukana kwa jina la Eduardo Mandai, alijitolea kumkamata mbwa huyo na kumtoa uwanjani. Wakati akiwa amemnyenyua mbwa huyo, alishitukia ameng'atwa lakini akalazimika kuendelea na mchezo.
Hili ni tukio la pili kwa mbwa kuvamia uwanja na siku chache zilizopita, tukio kama hilo lilitokea nchini Argentina. Msimu huu kule La Liga kwenye mechi kati ya Barcelona dhidi ya Elche, paka alivamia uwanja na baadae kutolewa.
Eduardo baada ya kurudi uwanjani, alifanikiwa kufunga bao la ushindi na kufanya timu yake ya Sao Pauolo kuchukua pointi tatu muhimu.
Baada ya mechi hiyo, mchezaji huyo alipost picha akiwa na mbwa huyo kwenye mtandao wa Instagram na kudai kuwa, kitendo cha kung'atwa na mbwa, ilikuwa ni bahati kwake kwani aliweza kuipatia timu yake goli la ushindi.
0 comments:
Post a Comment