Na Chikoti Cico.
Kocha
wa Arsenal Mfaransa Arsene Wenger anaonekana kukata tamaa kwenye mbio
za ubingwa wa ligi kuu nchini Uingereza, akiongea na waandishi wa habari
baada ya mchezo dhidi ya Swansea City ulioisha kwa Arsenal kufungwa kwa
magoli 2-1 Wenger alionyesha kutokuwa na matumaini ya kuwafikia vinara
wa ligi hiyo timu ya Chelsea ambayo mpaka sasa haijapoteza mchezo wowote
toka msimu uanze.
Arsenal ambao walikuwa wa kwanza kupata goli kwenye mchezo huo kupitia kwa Alexies Sanchez walishindwa kulinda goli hilo moja na kuwaruhusu Swansea kupata goli la kusawazisha lililofungwa na Gylfi Sigurdsson kwenye dakika ya 75 kabla ya Bafetimbi Gomis kuipatia Swansea goli la ushindi kwenye dakika ya 78.
Akiizungumzia timu ya Chelsea ambayo mpaka sasa inaongoza ligi ikiwa na alama 29 baada ya mchezo huo Wenger alisema “ Angalia msimu na Chelsea wanaelekea kupata alama 105, angalia namba ya alama walizonazo leo na kama wakiendelea hivyo hakuna atakayewagusa kwa hakika”
Aliendelea kusema “haionekani kama kuna mtu ana uwezo wa kushindana nao kwa sasa hakuna sababu ya wazi ila wamekuwa na mwanzo mzuri na kama usipopoteza mchezo huna haja ya kujiuliza maswali, labda hamasa kidogo zaidi kwenye timu huwasaidia wakati inapokuwa ngumu”
Huku akiwa na kumbukumbu mbaya ya kutoa sare ya 3-3 dhidi ya Anderlecht kwenye michuano ya ligi ya mabingwa Ulaya Wenger alisema “ Nafikiri ni ngumu kuelezea kivipi tulipoteza kuongoza wakati tulikuwa tumewashika lakini hawakukata tamaa, nafikiri tulipoteza umakini kwenye sehemu ya katikati ya uwanja kwenye dakika 20 za mwisho na ilitugharimu na ndipo tuliposhindwa mapigano”
Mpaka sasa Arsenal inashika nafasi ya sita kwenye msimamo wa ligi huku ikiwa na alama 17 hivyo kuwa na tofauti ya alama 12 dhidi ya vinara Chelsea ambao mpaka sasa wameshinda michezo tisa na kutoka sare michezo miwili hivyo kujikusanyia alama 29 katika michezo 11 ya ligi.

0 comments:
Post a Comment