Real madrid leo watawakaribisha mahasimu wao toka jiji la madrid Atletico madrid katifa fainal ya kombe la mfalme.Kocha josee Mourinho anataka kuwatuliza angalau mashabiki kwa kuchukuwa taji hili lakini Atletico nao watakuwa wanataka kumaliza uteja wao uliodumu kwa takriban miaka 14 tangu mara yao ya mwisho kumfunga Real Madrid mwaka 1999.
kuelekea mechi hii Mourinho anakabiliwa na changamoto kadhaa kwanza ni ugomvi wake na kipa Iker CASSILAS na kwasasa PEPE kaongezeka.Mourinho alianza kumbench Cassilas huku akidai ameshuka kiwango na Antonio Adan ni zaidi yake lakini kipindi cha uhamisho,akammnunua Diego Lopez na kumtumia kama kipa namba moja.Swali liliibuka kulikuwa na sababu gani ya kumnunua LOPEZ wakati alishakaririwa akisema ADAN anakiwango kikubwa?
hivi karibuni Mourinho ameingia kwenye malumbano na mreno mwenzie PEPE huku akimponda na kumwambia uzee ndo unamsumbua,anahaha kwa sababu MFARANSA dogo Rafael VARANE ndo habari ya mujini.VARANE aliumia kwenye mechi vs Espanyol na hatocheza leo je,MOURINHO atampanga pepe?
kikosi cha Real Madrid kinachoweza kuanza
1.LOPEZ 2.ESSIEN 3.COENTRAO 4.ALBIOL 5.RAMOS 6.ALONSO 7.DI MARIA 8.KHEDIRA
9.BENZEMA 10.OZIL11.RONALDO
Mourinho anapenda sana kutumia siku hizi mfumo 4-2-3-1 kwa namna hii Alonso na Khedira ndo watakuwa wakabaji huku RONALDO,OZIL na DI MARIA wakitumika kama viungo washambuliaji na BENZEMA kama strika pekee.
ATLETICO wataingia Dimbani kutaka kuvunja record yao mbaya dhidi ya mahasimu wao na pia wanaweza kunufaika na mgogoro bubu uliopo pale BERNABEU.Wanafaida ya kuwa na DIEGO COSTA ambaye ndiye anayeongoza kwa magoli kwenye kombe hili (7) na CR7 akiwa na (6) huku manne ya COSTA yakitokana na PENALTY huku moja la CR7 likiwa la penalty
Radamel FALCAO kama kawa atakuwa dimbani na hapa ndipo hali ya hewa inaweza kubadilika BERNABEU.Anajua sana kazi yake mkorombia huyu atakuwa na pacha wake DIEGO COSTA.Hawajamaa ukiwapa nafasi,unaweza lala mlango wazi.kumkosa VARANE ni pengo kwa madrid na pepe siku hizi kafulia,huyu Albiol sijui hata kapata mganga gani wakumfanya awe madrid.kiufupi,anastahili kuichezea QPR na sio MADRID.
Kwenye dimba la Atletico wanapenda kuweka watu wanne KOKE,GABI,SUAREZ na TURAN kwahiyo hapa utagundua kwamba madrid watataka kupata bao kwa counter attacks kama kawa kupitia pembeni huku,ATLETICO watapitia kati ambako ndipo wamejaza viungo.kwahiyo JUANFRAN beki wa kulia wa ATLETICO na LUIZ beki wa kushoto wanatakiwa kuwazui CR7 na DI MARIA wanaotokea pembeni huku,KHEDIRA na ALONSO wakiwazuia viungo wa ATLETICO.
hawa wanaweza anza upande wa ATLETICO
1.COURTOIS 2.JUANFRAN 3.LUIZ 4.GOLDIN 5.MIRANDA 6.KOKE 7.TURAN 8.GABI 9FALCAO 10.COSTA 11.SUAREZ
iwe itakavyokuwa,ubora wa RONALDO ndani ya dk 90 ndo utaamua BINGWA.
17 May 2013
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment