Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2014
Saturday, November 15, 2014

Hatimaye kocha atupiwa virago.



Claudio Ranieri atupiwa virago Ugiriki.
 
Na Chikoti Cico.

Wakati mechi za kuwania kufuzu michuano ya EURO kwa mwaka 2016 zikiendelea, kocha wa timu ya taifa ya Ugiriki Claudio Ranieri amefukuzwa kazi kuifundisha timu hiyo baada ya kuwa na matokeo mabovu toka alipoichukua timu hiyo katikati ya mwaka huu.

Shirikisho la mpira wa miguu nchini Ugiriki, HFF limefikia hatua hiyo baada ya timu yao ya taifa kuonyesha kupoteza mwelekeo kwani mpaka sasa wamefungwa mechi tatu kati ya nne za kufuzu michuano hiyo na kubakia mkiani kwenye msimamo wa kundi G wakiwa na alama moja.


Ranieri aliyechukua nafasi ya kocha wa zamani wa Ugiriki, Fernando Santos baada ya kombe la Dunia mwaka huu ameifundisha timu hiyo kwa muda wa miezi minne tu toka apewe kazi hiyo na shirikisho la mpira miguu la Ugiriki na kipigo cha goli 1-0 toka kwa timu ya taifa ya kisiwa cha Faroe, kilichangia kuondolewa kwa Ranieri.

Raisi wa HFF, Giorgos Sarris akiongea na mtandao wa shirikisho hilo alisema “Kufuatia matokeo mabovu ya timu ya taifa, nachukua majukumu yote kwa chaguo la kocha ambalo limesababisha taswira mbaya ya timu ya taifa mbele ya mashabiki"

"Utawala utakaa na kuchukua jukumu kwa wanachama wote kufanya mabadiliko ya lazima yanayohitajika kuepuka kujirudia kwa usiku ule wa aibu”

Ranieri ambaye amewahi kuzifundisha timu za Chelsea ya Uingereza na Monaco ya Ufaransa, atabaki kuifundisha timu ya hiyo kwa mara ya mwisho siku ya Jumanne kwenye mechi ya kirafiki dhidi ya Serbia kabla ya HFF kutafuta kocha mwingine wa kuifundisha timu hiyo ambayo ina nafasi ndogo ya kufuzu kwa michuano ya EURO kwa mwaka 2016.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!