Searching...
Image and video hosting by TinyPic
15 November 2014
Saturday, November 15, 2014

Stars dimbani leo Swaziland.


Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, leo kinashuka dimbani kumenyana na timu ya Taifa ya Swaziland katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la soka la kimataifa (FIFA), utakaopigwa kwenye uwanja wa Taifa wa Somhlolo, nchini Swaziland.


Mchezo huo ni muhimu kwa Stars kushinda ili kujiweka sawa kwenye viwango vya soka vya kimataifa vinavyoratibiwa na shirikisho hilo. Kwa Stars, mchezo huo ni muhimu ili kuifanya Tanzania iwezekuchumpa zaidi kwa nafasi kadhaa kwenye viwango vya FIFA.

Itakumbukwa kuwa ushindi wa 4-1 wa timu hiyo dhidi ya Benin Octoba 12 mwaka huu katika mechi ya kalenda ya FIFA ulitosha kuipaisha timu hiyo katika viwango hivyo kutoka nafasi ya 115 hadi 110 iliyo kwa sasa.

Wachezaji wa Stars wanapaswa kutambua kuwa, wanadhima kubwa kwa watanzania kwenye mchezo huo na hawapaswi kuichukulia mechi hiyo kama ya Bonanza, kwani kufungwa na Swaziland ambayo tunaizidi kwenye viwango hivyo ikiwa nafasi ya 164, kutatuporomosha kwenye viwango vya FIFA.

Stars kwa sasa inashika nafasi ya 110 katika viwango vya soka vya kimataifa ambayo bado haiipi hadhi Tanzania kulinganisha na nchi za Magharibi, ingawa inaishinda Swaziland kwa nafasi 54. 

Wakati tunawatakia ushindi kwenye mchezo huo dhidi ya Swaziland, jambo moja wanalopaswa kulitambua ni kuwa ushindi hauwezi kushuka kama mvua, bali kwa kila mchezaji kujituma dimbani katika kuupigania.

Source: Gazeti la Dimba, Jumapili.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!