Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 October 2014
Thursday, October 23, 2014

Ushoga kwenye soka la Uingereza

N a Oscar Oscar Jr

Kocha wa timu ya taifa ya Uingereza, Roy Hodgson amekana kuwahi kufanya kazi na mchezaji ambaye anashiriki mapenzi ya jinsia moja. Kocha huyo alikutana na swali hilo usiku wa jana wakati akizungumza na wanafunzi wa Cambridge Union.

Kocha huyo pia ameshindwa kukanusha uwepo wa watu wenye tabia kama hizo kwa sababu, wanapatikana kwenye kila nyaja hivyo ni vigumu sana kuwakosa kwenye mchezo wa soka. Hodgson amesema kuna uwezekano wapo ila wanaogopa kujiweza hadharani.

Mbali na swali hilo la ushoga, aliulizwa pia kuhusu uhusiano wake na kocha wa Liverpool, Brendan Rodgers kufuatia vuta nikuvute ya mchezaji Raheem Sterling lakini, Boss huyo alidai wako kwenye uhusiano mzuri na hakuna tatizo lolote.


0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!