Searching...
Image and video hosting by TinyPic
23 October 2014
Thursday, October 23, 2014

Mchezo mmoja wa Uefa kurudiwa.


Na Oscar Oscar Jr

KLABU ya Sporting Lisbon imepeleka malalamiko yao kwenye shirikisho la soka barani Ulaya (Uefa) wakilitaka shirikisho hilo liruhusu kurudiwa kwa mchezo baina yao na timu ya Schalke baada ya mtanange huo kupigwa siku ya Jumanne na Sporting kufungwa magoli 4-3.

Taarifa walioitoa leo Schalke imedai kuwa, Mwamuzi wa mchezo huo Mrusi Sergei Karasev alitoa penati isiyostahili dakika za lala salama kwa Schalke huku Eric-Maxim Choupo akifunga mkwaju huo na kuwapatia vijana hao wa Ujerumani alama tatu muhimu.

Mshambuliaji wa Schalke Klaas Juan Huntelaar amesema walikuwa na bahati sana katika mchezo huo ambao awali,walikuwa wanaongoza kwa magoli 3-1 kabla ya Sporting Lisbon kucharuka na kufanya matokeo kuwa 3-3 kablaa ya kupenati iliyozua utata kufungwa.

Uongozi wa Sporting Lisbon tayari umepeleka malalamiko yao Uefa yakutaka mchezo huo urudiwe au kifanyike chochote angalau matokeo yasomeka kama sare na sio kuwapa ushindi Schalke. Kinachosubiriwa kwa sasa ni uamuzi wa Uefa juu ya malalamiko ya timu ya Sporting Lisbon.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!