Ujio mpya wa Theo Walcott
Na Oscar Oscar Jr
Mchezaji wa kimataifa wa Uingereza na klabu ya Arsenal, Theo Walcott anatarajiwa kurudi dimbani ndani ya siku chache zijazo na hii ni baada ya kukaa nje kwa takribani miezi nane kufuatia kuumia kwenye mchezo wa kombe la FA mapema mwaka huu ambapo Arsenal ilicheza na mahasimu wao, timu ya Tottenham na kuibuka na ushindi.
Winga huyo machachari tayari ameanza kazi baada ya kucheza mwezi huu mechi moja kwenye kikosi cha U-20 cha Arsenal na siku ya Jumapili hii, atajumuika pia kwenye kikosi hicho ambacho kitacheza na timu ya Stoke City.
Kocha wa Arsenal mzee Arsene Wenger amedai kuwa hawezi kuhuharakisha Theo kurejea dimbani na tayari hajamjumuisha kwenye kikosi kitakacho safiri kwenda kupambana na Sunderland mwishoni mwa juma hili.
Matumaini ya Walcott kuwa sehemu ya kikosi cha kwanza yameongezeka kwenye mchezo wao utakao fuata dhidi ya Burnley utaopigwa kwenye dimba la Emirates weekend ijayo.
0 comments:
Post a Comment