Searching...
Image and video hosting by TinyPic
19 October 2014
Sunday, October 19, 2014

Uchambuzi: West Bromwich Albion vs Manchester United


Na Chikoti Cico

Ligi kuu ya Uingereza inatarajiwa kuendelea tena Jumatatu kwa mechi moja kati ya West Brom dhidi ya Manchester United, mechi itakayopigwa kwenye uwanja wa The Hawthorns nyumbani kwa West Bromwich Albion.

West Bromwich Albion wanaoishika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi wanatarajiwa kuwakosa Victor Anichebe na Silvestre Varela ambao ni majeruhi huku nahodha Chris Brunt akitarajiwa kuwa fiiti baada ya kuumia wakati akiichezea Ireland ya Kaskazini kwenye mechi za kimataifa.

Kocha wa West Bromwich Albion Alan Irvine ataingia kwenye mechi dhidi ya Manchester kutafuta ushindi wake wa pili nyumbani ili kujiweka kwenye nafasi nzuri ya msimamo wa ligi kuu.

Mpaka sasa kati ya mechi tatu walizocheza nyumbani toka kuanza kwa ligi ameweza kushinda mchezo mmoja, kufungwa mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja.

Takwimu zinaonyesha mshambuliaji wa West Brom Saido Berahino amefunga magoli sita kati ya mechi nane alizoichezea timu yake hiyo huku magoli matano yote akiyafunga kwenye uwanja wa the Hawthorns.

Wakati huo huo West Brom wamekuwa na rekodi mbaya kwenye mechi za Jumatatu kwani kati ya michezo 18 iliyopita waliyocheza siku ya Jumatatu wamepoteza michezo tisa na kushinda michezo miwili na kutoka sare michezo saba.

Wachezaji wa West Brom waliopo fiti kwa mechi ya leo: Foster, Myhill, Pocognoli, Gamboa, Dawson, Lescott, McAuley, Olsson, Davidson, Wisdom, Baird, Morrison, Mulumbu, Brunt, Blanco, Sessegnon, Samaras, Ideye, Berahino.

Kwa upande wa Manchester United kocha wa Luis Van Gaal ataendelea kumkosa Wayne Rooney anayetumikia adhabu pia atawakosa mabeki Jonny Evans na Paddy McNair na viungo Jesse Lingard na Antonio Valencia ambao ni majeruhi.

Lakini kurejea kwa Ashley Young, Phil Jones, Michael Carrick, Chris Smalling na Ander Herrera ambao walikuwa ni majeruhi kutaiongezea makali timu ya Manchester United hasa sehemu ya ulinzi na kiungo.

Manchester United wanaoshika nafasi ya tano wakiwa na alama 11 kwenye msimamo wa ligi watataka kufuta rekodi mbaya ugenini kwani mpaka sasa wameshindwa kushinda hata mechi moja kati ya michezo mitatu waliocheza ugenini huku wakipoteza mchezo mmoja na kutoka sare michezo miwili.

Katika mechi tano zilizopita za ligi zilizochezwa siku ya Jumatatu timu ya Manchester United imeshinda mchezo mmoja na kutoka sare mchezo mmoja huku ikipoteza michezo mitatu.

Wakati huo huo, Kiungo wa Manchester United Angel Di Maria toka amesajiliwa amehusika kwenye magoli sita huku akifunga magoli matatu na kutoa pasi tatu za magoli.

Kocha Van Gaal anategemea Di Maria atazidi kuimarisha safu ya kiungo cha United dhidi ya Wets brom. Wachezaji wa United walio fiti kwa mechi ya kesho: De Gea, Lindegaard, Amos, Johnstone, Rafael, Shaw, Rojo, Blackett, Thorpe, Smalling, Jones, Pereira, Blind, Fletcher, Fellaini, Anderson, Carrick, Young, Herrera, Mata, Januzaj, Di Maria, Falcao, Van Persie, W Keane.

Rekodi zinasema Manchester United na West Bromwich Albion wamekutana mara 116 kwenye ligi huku Manchester United wakishinda michezo 51 na West brom wakishinda michezo 38 na wametoksa sare michezo 27.

0 comments:

Post a Comment

 
Back to top!